.

.
.

.

.
.

.

.
.

.

.
.

.

.
.

.

.
.

.

.
.

Tuesday, August 26, 2014

Serikali yasisitiza katika uzalishaji,ukusanyaji na usindikaji wa Maziwa.

Msemaji wa Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi Dkt. Mohamed Bahari akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) walipotembelea kiwanda cha uzalishaji wa maziwa kilichopo Kigamboni jijini Dar es Salaam ambapo Serikali inasisitiza watanzania kuwekeza katika sekta ya ufugaji na uzalishaji wa maziwa ili kukuza uchumi.

Mkurugenzi wa kiwanda cha Maziwa cha MilkCom Dairies Ltd Yusuph Said akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari kuhusu bidhaa zinazozalishwa kiwandani hapo  wakati walipotembelea kiwanda hicho eneo la Kigamboni leo jijini Dar es Salaam.

Meneja Mkuu wa kiwanda cha maziwa cha MilkCom Dairies Ltd Bw. Cor van den Doel akitoa elimu kwa waandishi wa habari kuhusu mbinu bora wanazotumia kwenye  ufugaji  wa ng’ombe wa maziwa ambapo alisema kuwa kitaalam ng’ombe mmoja anaweza kutoa lita 40 za maziwa kwa siku.  


Baadhi ya ng’ombe  wanaofugwa kwa ajili ya uzalishaji wa maziwa kwenye kiwanda cha MilkCom Dairies Ltd kilichopo Kigamboni jijini Dar es Salaam. Zaidi ya ng’ombe 15,000 wanafugwa katika kiwanda hicho kwa ajili ya uzalishaji wa bidhaa zinazotokana na maziwa zikiwemo maziwa na mtindi.
(Picha na Georgina Misama)