JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
BUNGE MAALUM
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
RATIBA YA MKUTANO WA BUNGE MAALUM TAREHE 17 HADI 21 MACHI, 2014
Ofisi
ya Katibu wa Bunge Maalum inawatangazia Wajumbe wa Bunge Maalum na umma kwa
ujumla kuwa Mkutano wa Bunge Maalum utaendelea mjini Dododma kesho kwa ratiba
ifuatayo:
Tarehe
17/3/201 kuanzia saa 3:00 asubuhi kutakuwa na kiapo kwa Wajumbe wa Bunge Maalum ambao bado
hawajaapishwa. Hivyo Wajumbe wote ambao
hawajaapa kiapo cha ujumbe wa Bunge
Maalum wanatangaziwa kufika Idara ya Shughuli za Bunge Maalum kesho saa
2:00 asubuhi bila kukosa kwa ajili ya
kutambuliwa.
Saa
11:00 jioni Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Jaji Joseph Sinde
Warioba atawasilisha Rasimu ya Katiba
kwenye Bunge Maalum.
Tarehe
18/3/2014 kuanzia saa 3:00 asubuhi Wajumbe wote wa Bunge Maalum watapewa semina
kuhusu ufahamu mpana zaidi wa Kanuni za
Bunge Maalum.
Tarehe
19 na 20/3/2014 kuanzia saa 3:00 asubuhi wajumbe wote watapewa semina kuhusu Rasimu ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania.
Tarehe
21/3/2014 saa 3:00 asubuhi kutakuwa na uteuzi wa Wajumbe wa Kamati za Bunge
Maalum na saa 10:00 jioni Mgeni Rasmi
ambaye ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania atalihutubia Bunge kuashiria
ufunguzi rasmi wa Bunge Maalum.
Atakayeipata
taarifa hii amjulishe mwenzake.
Imetolewa na Ofisi ya
KATIBU WA BUNGE
MAALUM