.

.
.

.

.
.

.

.
.

.

.
.

.

.
.

.

.
.

.

.
.

Saturday, September 14, 2013

Tindikali tena Zanzibar ...

Padre Joseph Mang'amba  wa parokia ya Machui Zanzibar aliyemwagiwa tindikali na watu wasiyojulikana akisalimiana na Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Dkt. Mohamed Shein alipomtembelea hospitalini kumjulia hali. Umwagiaji watu tindikali (Concentrated Acid) kwa Zanzibar ni jambo la kawaida sasa. Na hakuna hatua zozote zinazochukuliwa

Dkt Mohamed Shein akimsikiliza Parde Mang'amba  huku akiwa katika maumivu makali na akiashiria kuwasamehe walifanya kitendo hicho. Huyu ni padre wa tatu wa kanisa Katoliki baada ya Padre Ambrose aliyemwagiwa tindikali na Padre Mushi aliyeuawa kwa kupigwa risasi. Yote ni matukio ya mwaka huu. Halikadhalika viongozi wawili wa ngazi za juu wa dini ya Kiislam nao wamemwagiwa tindikali mwaka huu

Waumini na watu wenye mapenzi mema waliofika kumpa pole Padre Mang'amba wazungumza na Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar. Pia mwezi uliopita waalimu wawili, wasichana wa kiingereza walimwagiwa tindikali wakiwa Zanzibar.