1. Spika wa Bunge la Jamhuri ya Korea Kusini wiki
iliyopita alihitimisha ziara ya siku
tatu hapa nchini aliyoianza tarehe 8 hadi 10 Julai 2013 ambapo alikutana na
viongozi wakuu wa Taifa. Awali alikutana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete, Spika wa Bunge la Tanzania Mhe. Anne S.
Makinda. Spika huyo pia akiambatana na Naibu Spika wa Bunge la Tanzania Mhe.
Job Ndugai aliizuru Zanzibar na kukutana na Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Dkt.
Mohammed Shein na Spika wa Baraza la Wawakilishi Mhe. A.P. Kificho. Katika
mazungumzo waliyofanya, jambo lililojikeza na kupokelewa kwa mtizamo chanya ni
lile la Tanzania kufungua Ubalozi nchini Korea. Pichani Spika wa Bunge la
Tanzania Mhe. Anne S. Makinda wa nne kushoto na Spika wa Bunge la Korea Mhe.
Kang Chang-Hee wa nne kulia wakiendesha mkutano baina yao na wabunge wa nchi
zote mbili ulifanyika jijini Dar es Salaam.
Wajumbe wa mkutano kwa upande wa Tanzania. |
Picha ya pamoja ya viongozi hao baada ya mkutano ambao baadhi ya mambo yaliyozungumziwa ni pamoja na Korea kuwekeza hapa nchini katika Nyanja ya TEHAMA. |
Spika Makinda akimkabidhi mgeni wake zawadi mara baada ya chakula cha jioni. |
Spika Kang akipokelewa na Spika wa Baraza la Wawakilishi Mhe. A.P. Kificho mara tu baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Zanzibar. |
Rais wa Zanzibar Dkt. Mohammed Shein (kulia) akiwa na mazungumzo na Spika wa Bunge la Korea Kusini Mhe. Kang Chang-Hee (kushoto). Katikati ni mkalimani. |
Picha ya pamoja kwenye Ikulu ya Zanzibar. |
Rais wa Zanzibar Dkt. Mohammed Shein akisalimiana na Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai (Mb) wakati wa ziara ya Spika wa Korea visiwani Zanzibar. |
Spika wa Bunge la Korea Kusini Mhe. Kang Chang-Hee akiushukuru ujumbe wa Tanzania kwa heshima kubwa mara baada ya kumaliza ziara yake hapa nchini. |