Mwenyekiti wa
Chama cha Mabunge ya nchi wanachama wa Jumuiya ya Madola (CPA) Tawi la Tanzania
Mhe. Mussa Zungu Azzan akifungua kikao cha
Kamati tandaji pamoja na Sekretarieti
jijini Dar es Salaam leo kujadili ushiriki wa Tawi la Tanzania katika Mkutano
Mkuu wa 44 wa CPA Kanda ya Afrika
utakaofanyika Windhoek, Namibia kuanzia tarehe 17-27 Julai, 2013. Kushoto kwake
ni Mratibu wa CPA Bwana Saidi Yakubu na Kaimu Katibu wa CPA Bwana Demetrius Mgalami.
Tanzania itakuwa mwenyeji wa
Mkutano Mkuu wa 45 wa mwaka 2014 ambapo Spika wa Bunge la Tanzania ambaye ni
Mkamu wa Rais wa CPA kwa sasa atachaguliwa kuwa Rais wa CPA Kanda ya Afrika.
|