.

.
.

.

.
.

.

.
.

.

.
.

.

.
.

.

.
.

.

.
.

Wednesday, July 31, 2013

KAMATI YA BUNGE YA KATIBA, SHERIA NA UTAWALA YAANZA KUKUTANA NA WADAU

 Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba, Sheria na Utawa Mhe. Pindi Hazara Chana na Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. William Ngeleja wakiendesha kikao cha kupokea maoni ya wadau mbalimbali kuhusu muswada wa sharia ya marekebisho ya sharia ya mabadiliko ya Katiba sura ya 83(2012) katika Ofisi ya Bunge, Dar es Salaam, leo.
 Wajumbe na wadau kutoka Asasi mbalimbali (zikiwemo WLAC, TAWLA, LHRC, TANLAP, TUCTA na TLS) waliohudhuria kikao hicho.



 Mhe. Tundu Lisu, Mjumbe wa Kamati akitoa ufafanuzi wa vifungu vya sharia.
 Mwanashria wa Mtandao wa Utoaji wa Msaada wa Kisheria Bi. Sarah Mkenda (TANLAP) akiwasilisha mapendekezo ya Asasi yake.
 Mjumbe wa Kamati Mhe.  Nyambali Nyangwini akichangia wakati wa mjadala na wadau.
 Mjumbe kutoka The Tanganyika Law Society (TLS) akiwasilisha mapendekezo ya Asasi hiyo.
Baadhi ya wadau waliofika kwenye mjadala huo.

Monday, July 22, 2013

THE OLD GOOD DAYS - 1

 Prof. Boos na Mkewe Kareen (cheers) na marafiki zao 1990-95

 Mimi na rafiki yangu Costantine Mgalle


 Kidato cha Sita Don Bosco 1991
 Marehemu Fr. James (mvi) na marafiki zake
Mimi na rafiki zangu

Tuesday, July 16, 2013

CPA tawi la Tanzania kuwa mwenyeji CPA kanda ya Afrika mwakani


Mwenyekiti wa Chama cha Mabunge ya nchi wanachama wa Jumuiya ya Madola (CPA) Tawi la Tanzania  Mhe. Mussa Zungu Azzan akifungua kikao cha Kamati tandaji pamoja na  Sekretarieti jijini Dar es Salaam leo kujadili ushiriki wa Tawi la Tanzania katika Mkutano Mkuu wa 44 wa  CPA Kanda ya Afrika utakaofanyika Windhoek, Namibia kuanzia tarehe 17-27 Julai, 2013. Kushoto kwake ni Mratibu wa CPA Bwana Saidi Yakubu na Kaimu Katibu wa CPA Bwana Demetrius Mgalami.

Tanzania itakuwa mwenyeji wa Mkutano Mkuu wa 45 wa mwaka 2014 ambapo Spika wa Bunge la Tanzania ambaye ni Mkamu wa Rais wa CPA kwa sasa atachaguliwa kuwa Rais wa CPA Kanda ya Afrika.


Wajumbe wakimsikiliza Mwenyekiti

Mjumbe wa Kamati na Mbunge wa Kilindi Mhe. Beatrice Matumbo Shelukindo akichangia wakati wa mjadala.

 Wajumbe wa CPA Tawi la Tanzania




Monday, July 15, 2013

Ziara ya Spika wa Bunge la Korea Kusini nchini Tanzania


1.   Spika wa Bunge la Jamhuri ya Korea Kusini wiki iliyopita alihitimisha  ziara ya siku tatu hapa nchini aliyoianza tarehe 8 hadi 10 Julai 2013 ambapo alikutana na viongozi wakuu wa Taifa. Awali alikutana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete, Spika wa Bunge la Tanzania Mhe. Anne S. Makinda. Spika huyo pia akiambatana na Naibu Spika wa Bunge la Tanzania Mhe. Job Ndugai aliizuru Zanzibar na kukutana na  Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Dkt. Mohammed Shein na Spika wa Baraza la Wawakilishi Mhe. A.P. Kificho. Katika mazungumzo waliyofanya, jambo lililojikeza na kupokelewa kwa mtizamo chanya ni lile la Tanzania kufungua Ubalozi nchini Korea. Pichani Spika wa Bunge la Tanzania Mhe. Anne S. Makinda wa nne kushoto na Spika wa Bunge la Korea Mhe. Kang Chang-Hee wa nne kulia wakiendesha mkutano baina yao na wabunge wa nchi zote mbili ulifanyika jijini Dar es Salaam.


   Wajumbe wa mkutano kwa upande wa Tanzania.

Picha ya pamoja ya viongozi hao baada ya mkutano ambao baadhi ya mambo yaliyozungumziwa ni pamoja na Korea kuwekeza hapa nchini katika Nyanja ya TEHAMA.

Spika Makinda akimkabidhi mgeni wake zawadi mara baada ya chakula cha jioni.

Spika Kang akipokelewa na Spika wa Baraza la Wawakilishi Mhe. A.P. Kificho mara tu baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Zanzibar.

Rais wa Zanzibar Dkt. Mohammed Shein (kulia) akiwa na mazungumzo na Spika wa Bunge la Korea Kusini Mhe. Kang Chang-Hee (kushoto). Katikati ni mkalimani.

Picha ya pamoja kwenye Ikulu ya Zanzibar.

 Rais wa Zanzibar Dkt. Mohammed Shein akisalimiana na Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai (Mb) wakati wa ziara ya Spika wa Korea visiwani Zanzibar.

Spika wa Bunge la Korea Kusini Mhe. Kang Chang-Hee akiushukuru ujumbe wa Tanzania kwa heshima kubwa mara baada ya kumaliza ziara yake hapa nchini.