|
Boda-Boda Iringa ikielekea kwenye Harambee ya kanisa ambapo Mhe. Edward Lowassa alikuwa mgeni rasmi jana |
|
Yaanguka mtaroni yajeruhi |
|
Heka heka ya majeruhi.... dereva wa bodaboda Jafet Aser akikimbizwa Hospitali |
|
Abira wake, Theresia Mapiu, ambaye ni muuguzi akifikishwa hospitali |
|
Jeraha la Muuguzi Theresia Mapiu aliyekuwa anawahi kwenye harambee ya kanisa la Overcomers FM |
|
Dereva wa bodaboda akisaidiwa na mwenzake |
|
Wauguzi hospitali ya rufaa Iringa wakipokea majeruhi |
|
Mhe. Edward Lowassa ( Kulia) aliyekuwa mgeni rasmi kwenye harambee hiyo uso kwa uso na tapeli la kutupwa |
Kijana ambae amekuwa akiwaliza watumishi mbali mbali wa
umma na watu binafsi kwa kutumia jina la waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu
sera na uratibu wa bunge kijana Jonathan Wiliam Lukuvi( si jina lake
halisi)amekamatwa katika hafla ya kanisa la Overcomers FM akitaka kumtapeli
waziri mkuu wa zamani Edward Lowassa kupitia harambee hiyo.
Kijana huyo aliingia katika ukumbi wa St.DOminic leo
katika harambee ambayo mgeni rasmi alikuwa ni Lowassa na kupita mbele na
kutumia kipaza sauti kuzungumza kuwa anaitwa JOnathan Wiliam Lukuvi na ni mtoto
wa waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu sera na uratibu wa bunge na kuwa amekuwa
akimpigia simu mara kwa mara Lowassa na hata katika mkutano wake wa Jangwani
jijini Dar es Salaam alipata kuzungumza na Lowassa na hivyo kuomba kutekelezewa
ombi lake la msaada ambao hakuutaja.
Kutokana na utambulisho huo baadhi ya watu waliopata
kutapeliwa na kijana huyo akiwemo mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya
Iringa waliweza kuguna hali iliyopelekea askari polisi kufunguka na kumtia
mbaroni kijana huyo ambae alikuwa akiweka mtego wa kumtapeli Lowassa na
viongozi wengine katika hafla hiyo .
Hata hivyo baada ya polisi kumtia nguvuni kijana huyo
baadhi ya watu waliotapeliwa waliweza kumtambua huku familia ya Lukuvi
iliyokuwemo katika ukumbi huo ikimkana katu katu kuwa hana hata chembe ya
familia na watu hawamtambui .
Kada wa CCM maarufu mkoani Iringa Godfrey Malenga Lukuvi
alisema kuwa kijana huyo amekuwa akitumia jina la waziri Lukuvi kuliza watu na
kuwa wengi wamekuwa wakilalamika kuhusu utapeli unaofanywa na kijana huyo na
kuwa tayari alipata kukamatwa na polisi ila alitolewa .
Kwa upande wake katibu wa mbunge jimbo la Isimani ambae
pia ni familia ya Lukuvi Bw Thom Malenga Lukuvi alisema kuwa amekuwa akipokea
malalamiko mbali mbali kutoka kwa watu mbali mbali ambao wamelizwa na kijana
huyo na kuwa siku zote alikuwa akiweka mtego ili kumnasa kijana huyo tapeli
japo hakufanikiwa kumpata.
Thom ambae yupo nje ya mkoa wa Iringa kwa shughuli za
kifamilia alisema kuwa alitamani sana kama angebahatika kumshuhudia kwa macho
kijana huyo tapeli ila kwa kuwa yupo nje ya mkoa atajitahidi kurudi mapema
mjini Iringa ili kumwona tapeli huyo.
Kwa upande wake mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya
Iringa Teresia Mahongo alimweleza mwandishi wa mtandao huu wa
www.matukiodaima.com kuwa pia kijana huyo alipata kufika ofisini kwake kwa
ajili ya kumtapeli na baada ya kumshtukia alimtafuta waziri Lukuvi kwa simu na
kuelezwa kuwa kijana huyo ni tapeli mkubwa .
Hata hivyo mwanahabari Gerald Malekela wa radio Nuru Fm
alisema kuwa kijana huyo alipata kufika studio za radio hiyo kwa ajili ya
kutapeli uongozi kwa kutumia jina hilo na kufika studi za radio hiyo huku akiwa
na barua inayosifia watangazaji na kuomba kusaidiwa zaidi kama mmoja kati ya
wasikilizaji .
Mtandao huu ulipata nafasi ya kumtafuta kwa njia ya simu
waziri Lukuvi ambae mbali ya kumkana kuwa hamtambui bado alisema kuwa amepata
kuwaliza watu mbali mbali kwa kutumia jina lake.
Lukuvi alisema kuwa tayari amepata kupokea malalamiko
kutoka kwa mkurugenzi wa Manispaa ya Iringa na kumwagiza kumtakata na kutaka
sheria ichukue mkondo wake.
"Mimi huyu kijana simtambui na wala si ndugu yangu
ila amekuwa akitumia jina langu kutapeli watu na tayari alikamatwa na polisi
kwa utapeli huo"
Mkuu wa mkoa wa Iringa Dkt Christina Ishengoma aliwaonya
watu wanaoendelea kutapeli wengine kwa kutumia majina ya viongozi ama namna
nyingine yeyote kuacha mara moja na kuwa akiwa kama mwenyekiti wa kamati ya
ulinzi na usalama ya mkoa hatakubali kuona matapeli hao wakiendelea kulizwa
watu kwa njia ya udanganyifu .
Hata hivyo aliwataka wananchi kujiepusha na wimbo hilo la
utapeli kwa kuwaripoti polisi watu wanaowashukia kuwa ni matapeli .
Akiwa tayari ametiwa nguvuni na Askari Kanzu
Picha zote kwa hisani ya Francis Godwin