.

.
.

.

.
.

.

.
.

.

.
.

.

.
.

.

.
.

.

.
.

Wednesday, January 30, 2013

TASWIRA KITAIFA

Mabweni ya shule za kata ni tatizo?

Mwajuma Ramadhi ni mwanafunzi wa kidato cha tatu katika Shule ya Sekondari ya Mkoma iliyoko katika Wilaya ya Newala Mkoa wa Mtwara, anayeishi katika nyumba ya kupanga iliyoko karibu ya shule ambayo anasoma kwa mwezi analipa kodi Tshs 2500.
Pia Athumani Hamza Mwanafunzi wa Kidato cha pili anayesoma katika shule ya sekondari ya Mnyambe iliyoko katika Wilaya ya Newala, naye anaishi katika nyumba ya kupanga kwa mwezi analipa kodi Tshs. 2000, Shuleni Mnyambe kuna bweni la kulala wanafunzi, lakini mzazi wake hana pesa ya kulipia bweni kwa mwaka Tshs.100,000 (Picha kwa hisani ya www.mkumbaru.blogspot.com)





 Maabara katika shule za kata ni tatizo?

Hicho ndio chumba cha darasa kinachotumika kama maabara katika shule ya sekondari Dr. Alex iliyoko katika Wilaya ya Newala katika Mkoa wa Mtwara, Wilaya hiyo ina shule za sekondari za kata 28 lakini kati ya hizo ni shule nne tuu ambazo zina majengo mbalimbali ya maabara nazo ni Nambunga, Newala day, Nangwanda na Mnyambe.





Maktaba shule za kata ni  tatizo?

Hiki ni moja ya chumba kinachotumika kama Maktaba ya shule ya Sekondari ya Nangwanda iliyoko katika Wilaya ya Newala Mkoa wa Mtwara, Wilaya hiyo ina shule za Sekondari za Kata 28 na jengo moja la Maktaba katika shule ya Sekondari ya Newala day.





 Ubunifu, ajira na kipato

Mpukuta ni Mlemavu wa Viungo kwa muda wa miaka 20 sasa, amepata ulemavu huo baada ya kuumwa miguu kwa miaka saba alivyopona ndio miguu hiyo ikawa haina nguvu ya kukanyaga chini, kwa sasa anatembea kwa kutumia mikono yake miliwi na miguu ikiwa inaburuza chini. Analinda ndoo na samaki wa wavuvi na wachuuzi katika soko la Feri na kujipatia kipato cha sh.2000/-hadi 2500/- kwa kila ndoo.





 "Kuchimba dawa" ni issue  nzito
Baadhi ya abiria wa kwenda Mikoa ya Kusini Lindi na Mtwara, wakijisaidia katika kichaka ambacho kipo karibu na barabara katika Kijiji cha Ikwiriri Wilaya ya Rufiji Mkoa wa Pwani. Aina hii ya "kuchimba dawa"  sio tuu kuchafua mazingira pia ni hatari kwa afya.





 Supu ya Pweza na heshima ya ndoa

Licha ya Pweza kutabiri mechi mbalimbali za mpira wa miguu katika Bara la Afrika na Ulaya, lakini supu ya Pweza inarudisha heshima ndani ya ndoa, kwa kunywa supu hiyo na mkia wake iliyopikwa vema kwa dakika 30 na kuwekwa viungo kama ndimu na tangawizi kukata shombo , ukinywa hiyo baada ya saa moja mambo safi ndani ya ndoa," anasema Mfaume Namkopi mpika na mkaanga pweza wa sokoni Feri kwa miaka 21 sasa.

Victar Mwandike ni Afisa Uvuvi wa Sokoni hapo alisema kuwa samaki jamii ya Kamba, Kitaa na Pweza wanaongeza vitamini A katika mwili wa binadmu na huleta heshima katika tendo la ndoa. na