.

.
.

.

.
.

.

.
.

.

.
.

.

.
.

.

.
.

.

.
.

Monday, September 3, 2012

Afrika na changamoto ya ukuaji wa miji na makazi


Spika wa Bunge la Tanzania Mhe.Anne Makinda, Naibu waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe Goodluck Ole Medeye pamoja na wajumbe kutoka Tanzania wakifuatilia ufunguzi rasmi wa Mkutano wa 6 wa kuboresha miji na makazi mjini Napoli Italia leo. Katika mkutano huo, Umoja wa Mataifa umeweka bayana kuwa hakuna njia ya mkato ya kukabilina na changamoto za kukuwa kwa miji zaidi ya kuwa na sera madhubuti za kuboresha na kupanua miji. Mwanzoni mwa karne ya 20 ni 2% tu ya watu ilikuwa ikiishi mijini. Leo ni 50%.



Spika Makinda na Mh. James Lembeli kwenye kikao cha kuwaelimisha watunga sharia, sera na mipango miji.



Mhe. Ole Medeye kwenye kikao cha matumizi ya ardhi na ongezeko la watu katika miji ya Afrika



Spika Makinda akishauriana jambo na Mhe. Ole Medeye (kushoto) na Naibu Katibu Mkuu  TAMISEMI



Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam Mhe. Masaburi akimsikiliza kwa makini Spika wa Bunge mara kabla ya kuanza kwa mkutano maalum wa mameya kuhusu ujenzi wa miji na makazi,


Wadau kwenye Mkutano huo.


Mwandaaji wa mkutano ( Volunteer)


Wadau mbalimbali wa mkutano









Sunday, September 2, 2012

Mji mpya wa Kigamboni wawa kivutio mkutano wa Miji na Makazi


     Spika wa Bunge la Tanzania Mhe. Anne Makinda (kushoto) akiwa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Bi. Maria H. Bidila, Bolozi wa Tanzania nchini Italia, Dkt. James Alex Msekela na Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi , Mhe. Goodluck Ole Medeye -  wakipeana msimamo wa kitaifa mara kabla ya kuanza kwa Mkutano wa 6 wa miji na makazi ulimwenguni, mjini Napoli Italia leo. Zaidi ya nchi 150 zinatajia kudhuria mkutano huo.



  Banda la maonesho la Tanzania katika ukumbi wa mkutano huo.



     Spika Makinda akipokelewa na kukaribishwa na maafisa waandamizi wa Wizara ya Ardhi, Numba na Maendeleo ya Makazi katika banda hilo.



  Balozi Msekela na Spika Makinda wakipata maelezo ya ujenzi wa mji wa Kigambo ambao umekuwa moja ya kivutio kikubwa katika maonesho haya.


  Ramani za mji mpya wa Kigamboni katika picha


      Afisa Mratibu wa Shirka la Makazi la Umoja wa Mataifa akiwa katika wakati mgumu baada ya kutoa nyaraka zilizolichanganya jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na la nchi ya Kenya. Spika wa Bunge, Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi pamoja na Balozi wa Tanzania nchi Italia kwa kauli moja wameuagiza uongozi wa shirika hilo kuomba radhi kwa maandishi (note verbale)na hadharani mara moja, jambo ambalo maafisa husika wamekubali kulitekeleza.



       Naibu waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Goodluck Ole Medeye (kati) pamoja na Bolozi wa Tanzania nchini Italia Dkt J. A. Msekela (kushoto) wakiwa na mazungungumzo na Mkurugenzi Mkuu wa International Ecological Safety Cooperative Organization Profesa Jiang Mingjun alipolitembelea banda la Tanzania.

Mhe, Ole Medeye na Prof Jiang Mingjun




  Balozi Msekela na Mhe. Susan Lyimo mjini Napoli




  Mkukutano unalega kuzungumzia matumizi rafiki ya mazingira. Hizi ni baadhi ya samani za maboxi/karatasi kwenye maonesho




Samani hizi zinafaa kwa matumizi ya nyumbani na ofisini




Spika Makinda akisaini kitabu cha wageni mashuhuri








Baadhi ya Wajumbe wa Bunge la vijana katika mkutano huo wakiwa kwenye picha ya pamoja na Spika wa Tanzania





Gari linalotumia betri kuepusha uchafuzi wa mazingira> gari hili pia kwa udogo wake hupunguza msongamano




Mazingira unamofanyika mkutano






Wadau kando ya stadium ya Napoli



Saturday, September 1, 2012

Spika Makinda awasili Italia kwenye mkutano wa makazi ulimwenguni

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Anne Makinda (kulia) akiwasili katika uwanja wa ndege wa Napoli, Italia na kulakiwa na mwenyeji wake, Balozi wa Tanzania nchini Italia, Dkt James Nsekela leo. Mhe. Makinda yuko nchini Italia kuhudhuria mkutao wa Shirika la Makazi la Umoja wa Mataifa unaohusu jinsi ya kukabiliana na ukuaji wa miji ulimwenguni. Hivyo zinahitajika juhudi za makusudi ili kuweka mipangilio stahihiki katika miji ya Tanzania hususan majiji ya Dar es Salaam, Mwanza na Mbeya, ikiwa ni pamoja na kuimarisha miundombinu ya usafirishaji. Ni hivi majuzi ilitangazwa kuwa Dar es Salaam ni miongoni mwa miji inayokuwa kwa kasi kubwa barani Afrika. Ujumbe wa Tanzania katika mkjutano huu unaongozwa na naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Goodluck Ole Medeye.Mkutano huo utaanza kesho tarehe 2 na kuhitimishwa tarehe 6 septemba 2012.
 
Spika Makinda katikati pamoja na baadhi ya watanzania wanaoishi Italia: kutoka kushoto ni Mhadhiri wa chuo Kikuu cha Napoli ambaye makamu Mwenyekiti wa Jumuiya ya Watanzania wanaoishi Napoli Italia Bi Fatma Tandika, Mwenyekiti wa jumuiya ya watazania wanaoishi Napoli, Balozi wa Tanzania nchini Italia Dkt. James Nsekela na Afisa mwandamizi katika Ubalozi wa Tanzania nchini Italia Bw. Msemo. 


Wadau ndani ya Emirate Air Bus A-380 Kutoka Dubai kwenda Roma, Italia wakiwa na mwenyeji wao Bi Haruka.