Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Anne Makinda, Mb |
Spika wa Bunge la Tanzania Mhe.
Anne S. Makinda (Mb) yuko Maputo Msumbiji kuhudhudhuria mkutano wa 31 wa Jukwaa
la Mabunge ya nchi wananchama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusinin mwa Afrika-
SADC-PF. Mkutano huo ulionza leo tarehe 11 Julai 2012 utajadili pamoja na mambo
mengine uwezekano wa kuunda Bunge la SADC. Jambo lingine linalojadiliwa katika
mkutano huo ni pamoja na kuimarisha demokrasia katika chaguzi mbalimbali za
nchi wanachama.
Tayari chombo hiki (SADC-PF) kimeanzisha
utaratibu wa kusimamia chaguzi mablimbali na kutoa taarifa iwapo katika chaguzi
hizo kumekuwa na ukiukwaji wa sheria na taratibu za uchaguzi.
Katika mkutano huo Tanzania
imepwa jukumu la kujifunza muundo na uendeshaji wa Bunge la Afrika Mashariki.
Wakati huo huo Afrika Kusini imepwa jukumu la kujifunza muundo na utendaji wa
Bunge la Umoja wa Ulaya. Nchi hizi mbili zitawasilisha taarifa kwenye kikao cha
SADC-PF kitakachofuata ili kuona ni kwa jinsi gani Bunge hilo litakavyoweza
kuundwa.
SADC-PF imekuwa mstari wa mbele
kutoa misaada na kuelimisha umma kuhusu virusi na kuishi na virusi vya UKIMWI
na kujikinga na maambukizi mapya UKIMWI. Aidha chombo hiki kimeshatoa mwongozo
wa kisheria kuhusu UKIMWI na jinsi ya kuuhamasisha umma.
Katika Mkutano huo Spika Makinda
naongoza ujumbe wa wajumbe watano ambao ni: Mhe. Stella Manyanya, Mhe. Anna
Abdallah, Mhe. Habib Mnyaa, Mhe. Titus Kamani na Kaimu Katibu wa Bunge Bwana Jossey
Mwakasyuka.