Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete akilihutubia taifa kwenye kilele cha Siku wa Wafanyakazi duniani ambapo pamoja na mengine aliahidi kuboreshwa kwa maslahi pamoja na kuwajibishwa kwa waliotajwa kwenye taarifa ya CAG jijini Tanga jana.
Wafanyakazi wa Ofisi ya Bunge katika muonekano wa kikao cha Bunge: "Spika" akitoa mwongozo, "PM" akijibu maswali ya papo kwa papo na "Katibu" akiwa anafuatilia kwa makini, wakipita mbele Rais wakati wa maadhimisho ya Mei Mosi
Wafanyakazi Mei Mosi: Kauli mbiu..... Mfumuko wa Bei, Mishahara kidogo, maisha magumu
Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani Tanzania Dkt Joyce Ndalichako akitoa takwimu za matokeo ya mitihani ya Kidado cha Sita jana. Ufaulu kwa mwaka huu 2012 umeongezeka kwa asilimia 0.34 ikilinganishwa na mwaka uliotangulia.