.

.
.

.

.
.

.

.
.

.

.
.

.

.
.

.

.
.

.

.
.

Wednesday, November 9, 2011

Balozi wa Umoja wa Ulaya amaliza muda wake Tanzania


Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Mizengo Pinda(kushoto)  na Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda (katikati) wakisalimiana na kubadilishana mawazo na Balozi wa Umoja wa Ulaya hapa Tanzania Mhe. Tim Clarke mjini Dodoma leo. Mhe. Tim Clarke amekuja Dodoma kuliaga Bunge baada ya kuwa hapa nchini kwa miaka minne.


Spika Makinda akiwa na mazungumzo ba Balozi Clarke ofisini kwake leo.

Ziwadi ni ishara ya ukarimu….Spika wa Bunge akimpa Balozi Clarke zawadi ya saa ya ukutani yenye jengo la Bunge la Tanzania.

Balozi Clarke(kulia) pia alikutana na kujadili masuala kadhaa na  Mwenyekiti wa kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama Mhe. Edward Ngoyai Lowassa (katikati). Kushoto ni mjumbe wa Kamati hiyo Mhe. Khalifa Khalifa.

Kutoka kulia ni Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama Mhe. Mussa Zungu Azzan, Bolozi wa Umoja wa Ulaya Tim Clarke, Mwenyekiti wa Kamati Mhe Edward Lowassa na Mjumbe wa Kamati  Mhe. Khalifa S. Khalifa.