|
Kilimo cha Chai Njombe |
Mkoa mpya wa Njombe umejiandaaje? (Na Prosper Minja)
Jamii maskini kwa kawaida huwa na vipaumbele vingi. Matokeo yake ni kushindwa kuvitekeleza. Wananchi wa mkoa mpya wa Njombe ambao ni wachapa kazi kweli kweli wameikataa falsafa hiyo na wamejiwekea vipaumbele vichache na vya uhakika ili kuujenga mkoa wao. Vipaumbe vya wananjombe ni:
1. Elimu- Kwa kujitolea wananchi wa vijiji na kata za Katulila, Madobole, Miva, Lusitu, Mtila, Mbega, Matola, Luponde, Itulike, Ramadhani, Kihesa, Utalingolo, Ihalula, Nolle, Mamongoro, Makowo, Ng’elamo, Yakobi, Igominyi, Idunda, Idihani, Lugenge na Kiyaula wameamua kujikita katika suala zima la elimu kwa shule za awali, msingi na sekondari. Majenfo mzuri ya ya kisasa yako katika hatua mbali mbali. Ombi lao ni waalimu wa kutosha.
2. Afya: Ili kuimarisha afya wananchi hao wako katika mpango wa kuwa na zahanati katika kila kata. Tayari kwa kujitolea wameanza ujenzi wa zahanati hizo. Ombi lao ni kupatiwa wauguzi wa kutosha.
3. Kilimo: kutokana na hali ya hewa nzuri ya nyanda za juu kusini, wananjombe hawa wamejizatiti katika kilimo cha chai, mahindi, viazi mviringo na misitu ya mbao.
4. Miundombinu: kwa sehemu kubwa wananjombe wamejitahidi sana kutengeneza barabara za ndani na wanaamini ni kwa barabara nzuri wataweza kufaidika na fursa zitokanazo na migodi ya machimbo ya chuma na mkaa wa mawe ya Mchuchuma na Liganga
|
Jengo la SACOSS Kata ya Utalingolo |
|
Wananjombe kwenye mkutano wa Hadhara |
|
Kituo cha Afya - Ihalula (Ujenzi upo katika hatua za mwisho) |
|
Misitu ya Mbao - Njombe |
|
Ujenzi wa Zahanati kijiji cha Nolle |
|
Mbunge wa Njombe Kusini Mhe. Anne Makinda akiweke jiwe la msingi katika Zahanati ya kijiji cha Utalingolo |
|
Ujenzi na ukarabati wa shule ya msingi Mbega |
|
ujenzi wa zahanati |
|
Ujenzi wa mabweni ya wanafunzi wa shule za sekondari (ufadhili wa kampuni ya Chai) |
|
Wananchi wenye ari ya kujenga mkoa wao |
|
Majengo ya Zamani- kumbukumbu za walikotoka wananjombe |
|
Usanifu mpya wa majengo |
|
Wananchi wakipata elimu ya Bunge kwa njia ya vipeperushi |
|
Vijana wa Njombe kusini wakimsikiliza na kumuuliza maswali Mbunge wao katika kata ya Matola |
|
wanafunzi wa sekondari ya matola wakiweka bayana mikakati yao ya masomo, huku Mbunge wao akiwasikiliza kwa makini |
|
Kipaumbele ni elimu |
|
Sura za kazi |
|
Spika wa Mhe. Anne Makinda akikata utepe kuashiria ufunguzi wa nyumba ya mganga- Makowo |
|
Wakati wa kusubiri madawati ya kisasa hakuna haja watoto kukaa chini - Ubunifu |
|
Taifa la kesho- urithi pekee ni eleimu |
|
Sekondari za kata mkoani Njombe-Hapa ni kitulila |
|
Vyumba vya kupumzisha wagonjwa katika zahanati ya Miva- ujenzi unaendelea |
|
Wanafunzi wenye ari na masomo |
|
Muonekano wa mabweni ya wanafunzi |
|
Ujenzi wa zahanati Mtila |
|
Zahanati Mtila |
|
Majengo ya Madara ya kisasa |
|
Majengo ya shule ambayo sasa wananjombe wameamua kuachana nayo |
|
Nyumba za waalimu |
|
Jengo la ofisi ya waalimu -nguvu za wananchi |
|
Hapa umeingia St Benedict Academy-Kipimo cha ukakamavu |
|
St Benedict |
|
Kihesa |
|
Wananchi wa Kihesa wakimsiliza Mbunge wao wa Njombe Kusini |
|
Taswira ya mkoa mpya wa Njombe |
|
Watoto wa shule ya awali wakitoa ujumbe wa UKIMWI kwa Spika wa Bunge |
|
Mhe. Makinda akiweka jiwe la msingi katika zahanati ya Kiyaula |