.

.
.

.

.
.

.

.
.

.

.
.

.

.
.

.

.
.

.

.
.

Friday, July 1, 2011

Bunge lawapongeza waliofanya vizuri kidato cha sita


Mpambe wa Bunge akiwaingiza Bungeni wanafunzi 20 kutoka shule
mabalimbali za Tanzania waliofanya vizuri katika masomo ya sayansi.
Ni wasichana kumi na wavulana kumi


Waziri Mkuu Mhe. Mizengo Pinda akiwakaribisha rasmi Bungeni
wanafunzi hao baada ya Kanuni ya 150 kifungu 2 kutenguliwa


Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Mhe. Shukuru Kawambwa akitoa
salamu za pongezi kwa wanafunzi hao, waalimu pamoja na wazazi wao.

Ndipo ulipotimia wakati wa kuwatunuku vyeti maalum vya kutambua
 juhudi zao. Waziri Mkuu Mhe. Mizengo Pinda, Spika wa Bunge
Mhe. Anne Makinda na Kiongozi wa Upinzani Bungeni Mhe.
Freeman Aikaeli Mbowe waliifanya kazi hiyo huku ukumbi
mzima wa Bunge ulilipuka kwa makofi, nderemo na vifijo.









Sekondari za Kata zaanza kuzaa matunda. Wahitimu saba waliofanya vizuri
 kidato cha sita wakitokea katika shule za sekondari za kata kwa kidato cha nne

Wahitimu wakipokea nasaha za Mhe. Spika. Hawa ni: Mhuhagachi Chacha
(Kibaha Sec), Susana Makoi (Tarakea), Mariam Matovolwa (Kilakala), Rahabu
Mwang'amba (Kilakala), Cecilia Mville (Kifungilo Girls), Mary Moshi
(Kifungilo Girls), Anthonia Lugumo (Usongwe Sec.), George Assenga
 (Majengo Sec),Catherine Temu (Ashira Girls), Samuel Katwale (Mzumbe),
Amir Abdallah (Feza Boys), Kudra Baruti (Feza Boys), Comman Nduru
 (Feza Boys),Aron Gerson (Tabora Boys), Shaban Omary (Tabora Boys),
Francis Joseph (Tabora Boys), George Felix (Benjamin Mkapa),
 Nuru Kipato (Marian Girls), Zainab Hassan (Al-Muntazir Islamic)

Wakisubiri kwa shahuku kubwa kuingia katika ukumbi wa Bunge

Hivi huko ndani kukoje ....?