Shirika la Maendeleo
la Umoja wa Mataifa (UNDP) kupitia mradi wake wa kuwawezesha Wabunge (LSP) hivi
karibuni limemkabidhi Spika wa Bunge Mhe. Anne Semamba Makinda (kwa niaba ya
Ofisi ya Bunge) gari aina ya Land Cruiser V8 baada ya kuridhishwa na utaratibu
mzuri wa Ofisi ya Bunge katika kuusimamia mradi huo. Gari hilo lenye thamani ya
shilingi milioni 96 litatumika katika miradi ya kuwajengea uwezo waheshimiwa
wabunge pamoja na watumishi wa Ofisi ya Bunge. Makabidhiano hayo yalifanyka
katika Ofisi ya Bunge mjini Dodoma mbele ya Makamishna wa Bunge pamoja na
Maafisa wa ngazi za juu wa Ofisi ya Bunge.
|