.

.
.

.

.
.

.

.
.

.

.
.

.

.
.

.

.
.

.

.
.

Tuesday, April 7, 2015

Kumbe inawezekana.... Ni Mtanzania halisi Chef Issa Kapande Mpishi maarufu duniania amefanikiwa kufungua mgahawa mkubwa wa kiafrika barani Ulaya. Mgahawa umefunguliwa jijini Trollhattan, Sweden na Balozi wa Tanzania nchini Sweden Mhe. Dora Msechu akiambatana na Meya wa Jiji la Trollhattan, Mhe. Paul Akerlund. Ni jitihada, ni kujituma, ni kujiamini ndiko kulikomfanya Bw. Kapande kufanya mambo ambayo wengi wanadhani hayawezekani....ughaibuni siyo tu kuajiriwa bali kujiajiri na kuajiri watu.....amefanya kazi katika nchi 17 duniani


Kukata utepe..... Mmiliki Bwana Kapande (shati jeupe) nyuma yake ni mkewe ambaye ndiye msukumo mkubwa.... kutoka kushoto ni Meya wa Trollhattan, Paul Akerlund na Balozi wa Tanzania nchini Sweden Mhe. Dora Msechu


Katika kazi yake ya upishi, amebahatika kuwapikia watu mashuhuri duniani, baadhi wakiwa Andrew Young, Mchungaji Jesse Jackson, Robert Mugabe (Rais wa Zimbabwe), Paul Kagame (Rais wa Rwanda), Benjamini Mkapa (Rais mstaafu wa Tanzania), Raila Odinga (Waziri Mkuu wa zamani wa Kenya), Daniel Arap Moi (Rais Mstaafu wa Kenya), Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Bi. Hillary Clinton na mumewe Bill Clinton,  Mke wa Rais wa zamani wa Marekani Laura Bush.
Wengine ni Rais wa Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein, mwigizaji Chris Tucker, Rais wa zamani wa Afrika Kusini hayati Mzee Nelson Mandela, Koffie Olomide, Youssour ndour, Arsene Wenger (Kocha wa Arsenal ya England), Gianluca Vialli (nyota wa zamani wa Italia aliyewahi kuichezea na kuinoa Chelsea ya England), Rais wa Congo DRC, Joseph Kabila, Billy Gates na wengine wengi.