JAMHURI YA
MUUNGANO WA TANZANIA
BUNGE LA
TANZANIA
TAARIFA KWA
VYOMBO VYA HABARI
Spika wa Bunge la Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Mhe. Anne Semamba Makinda (Mb) anatarajia kurejea
nchini siku ya Alhamisi tarehe 30 Januari 2014 akitokea Geneva, Uswisi alikoenda
kuhudhuria mkutano wa kwanza wa Kamati ya Maandalizi ya Mkutano wa Nne wa
Maspika Duniani utakaofanyika mwishoni mwa mwaka 2015. Kamati hiyo inayoundwa
na Maspika 37 walioteuliwa na Rais wa
Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) imekutana tarehe 27 – 28 Januari 2014 kwenye
Makao Makuu ya Umoja wa Mabunge Duniani Mjini Geneva. Mkutano wa pili wa Kamati
hiyo ya Maandalizi utafanyika mwishoni mwa mwaka huu.
Aidha, kabla ya kwenda Geneva,
Mhe. Spika alihudhuria mkutano wa 22 wa Maspika wa Mabunge ya Nchi wanachama wa
Jumuiya ya Madola (CPA) uliofanyika Wellington, New Zealand kuanzia tarehe 22
hadi 24 Januari 2014.
Kwa ujumla, ushiriki wa
nchi kwenye Mikutano ya Kimataifa huwa fursa nzuri ya kuitangaza na kuipa
heshima nchi yetu. Vile vile Mikutano hiyo huwa jukwaa madhubuti linalotumika
kuiweka nchi katika ramani ya dunia na kuonyesha vivutio hususan katika nyanja
za uwekezaji, utalii na maliasili pamoja na fursa mbalimbali zilizomo.
Imetolewa na:
Idara ya Habari, Elimu kwa Umma na
Uhusiano wa Kimataifa,
Ofisi ya Bunge,
DAR ES SALAAM
28 Januari 2014