Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete kwa mamlaka aliyo nayo kikatiba amamteua aliyewahi kuwa waziri wa Mambo ya Nje na Ushikiano wa Kimataifa na Naibu Katbu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Dkt Asha-Rose Migiro kuwa Mbunge. Uteuzi huo ulioanza tarehe 2 Disemba 2013 ulitangazwa na Kaimu Katibu Mkuu Kiongozi Dkt. Florens Turuka jana tarehe 3/12/2013 Ikulu Dar es Salaam. Dkt Migiro ni Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (CCM) Idara ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa. Huyu anakuwa ni mbunge wa nane wa kuteuliwa na Rais.
|