KAULI YA SERIKALI BUNGENI KUHUSU MLIPUKO ULIOTOKEAKATIKA KANISA KATOLIKI LA MTAKATIFU JOSEPH PAROKIA YAOLASITI, ARUSHA MJINI TAREHE 5 MEI, 2013
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Dk. Emmanuel Nchimbi
Mheshimiwa Spika,
kwa mujibu wa Kanuni ya 49 (1) ya Kanuni zaKudumu za Bunge, Toleo la Aprili, 2013, naomba kuwasilisha Taarifa yaawali kuhusu tukio la mlipuko uliotokea katika Kanisa Katoliki la MtakatifuJoseph Mfanyakazi, Parokia ya Olasiti, Jijini Arusha tarehe 5 Mei, 2013 saa4:30 asubuhi.
Mheshimiwa Spika,
mnamo tarehe 5 Mei, 2013 saa 4:30 asubuhikulitokea mlipuko katika kanisa Katoliki la Mtakatifu Joseph Mfanyakazi,Parokia ya Olasiti, jijini Arusha. Mlipuko huo ulitokea muda mfupi baada yakuanza kwa ibada ya uzinduzi wa Parokia. Mgeni Rasmi katika uzinduzialikuwa ni Balozi wa Vatican nchini na Mjumbe wa Baba Mtakatifu, AskofuFransisco Mantecillo Padilla. Aidha, alikuwapo mwenyeji wake AskofuJosephati Lebulu wa Jimbo Kuu Katoliki Arusha. Katika uzinduzi huoinakadiriwa kuwa kulikuwa na zaidi ya watu 2000. Wakati Mgeni Rasmiakiwa ametoka nje ya Kanisa akijiandaa kukata utepe kama ishara yauzinduzi mtu alirusha kitu chenye ukubwa wa ngumi kuelekea eneo kulipokuwa na mkusanyiko wa watu ambapo baada ya kutua kulitokeakishindo na mlipuko mkubwa. Mlipuko huo ulisababisha taharuki miongonimwa waumini na kusababisha watu kukimbia ovyo.
Mheshimiwa Spika,
katika tukio hilo watu wawili wamefariki duniaambapo REGINA LONGINO KURUSEI, Mwarusha, umri wa miaka 45, mkaziwa Olasiti alifariki dunia siku ya tukio wakati akipatiwa matibabu katikaHospitali ya Mount Meru na majeruhi mwingine JAMES GABRIEL umri wamiaka 16 amefariki dunia usiku wa kuamkia tarehe 6 Mei, 2013. Aidha,watu 59 wamejeruhiwa na watatu kati yao ni mahututi. Majeruhi 38walikimbizwa hospitali ya Mount Meru kupatiwa matibabu. Majeruhi 16walikimbizwa hospitali ya St. Elizabeth kwa Father Babu, majeruhi mmojaalipelekwa hospitali ya Selian na majeruhi mwingine alipelekwa katikahospitali ya Dkt. Wanjara, Mianzini. Natumia fursa hii kutoa pole kwawafiwa, uongozi wa kanisa Katoliki, wakazi wa Arusha na Watanzania wotekwa tukio hili la kinyama. Aidha, nawaombea majeruhi wote wa tukio hilowapone haraka.
Mheshimiwa Spika,
Viongozi wa dini na Serikali waliohudhuria ibada hiyohawakupata madhara yeyote kufuatia mlipuko huo. Baada ya Jeshi la PolisiMkoa wa Arusha kupokea taarifa ya tukio hilo waliimarisha ulinzi kwakuongeza idadi ya askari katika eneo hilo. Aidha, Kamati ya Ulinzi naUsalama ya Mkoa ikiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha MheshimiwaMagesa Mulongo walifika eneo la tukio na kufanya tathimini ya hali ilivyona kuelekeza hatua za kuchukuliwa.
Mheshimiwa Spika,
kutokana na uzito wa tukio hilo, kitaifa na kimataifa,Makamu wa Rais Mheshimiwa Dkt. Mohamed Gharib Bilal, Naibu Waziri waMambo ya Ndani ya Nchi, Mheshimiwa Pereira A. Silima, na InspektaJenerali wa Polisi, Said A. Mwema walikwenda Arusha na walitembeleaeneo la tukio, waliwatembelea majeruhi na kuelekeza hatua za ziada zakuchukuliwa.
Mheshimiwa Spika,
Uchunguzi wa awali unaonyesha kuwa mlipuko huoni bomu. Uchunguzi wa kubaini aina ya bomu lililotumika unaendeleakufanywa na Jeshi la Polisi na Wataalamu wa Jeshi la Wananchi waTanzania. Hadi sasa watuhumiwa sita wanashikiliwa na Jeshi la Polisi.Miongoni mwao ni Victor Calisti Ambrose
mwenye umri wa miaka 20,dereva wa bodaboda , mkazi wa Kwa Mrombo, Arusha ambayeanatuhumiwa kwa kurusha bomu hilo. Watuhumiwa wengine watanowaliokamatwa ni raia wanne wa kigeni na Mtanzania mmoja ambaowanashikiliwa kwa mahojiano.
Mheshimiwa Spika,
siku za karibuni kumekuwepo jitihada kubwa sana zawatu wachache wasiyoitakia mema nchi yetu kutaka kupandikiza chuki zakidini miongoni mwa watanzania na kuleta mapigano na mauaji miongonimwa watanzania, sina shaka kuwa shambulio la Arusha ni sehemu yamikakati hiyo miovu. Nataka niwahakikishie Watanzania kuwa Serikalihaitavumilia hata kidogo mbegu za chuki za kidini miongoni mwawatanzania na tutachukua hatua kali bila huruma kuzigandamiza njama hizimbaya dhidi ya taifa letu. Tutachukua hatua kali kwa mtu yeyote bila kujalihadhi na nafasi yake katika jamii. Amani yetu kwanza na taifa letu kwanza.
Mheshimiwa Spika,
Pamoja na kukamatwa kwa watuhumiwa hao, Waziriwa Mambo ya Ndani ya Nchi na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifawametoa maelekezo kwa Vyombo vya Ulinzi na Usalama ambapo tayariInspekta Jenerali wa Polisi kwa kushirikiana na Wakuu wa Vyombo vinginevya Ulinzi na Usalama wameunda Kikosi Kazi maalumu ili kuchunguza tukiohilo.
Mheshimiwa Spika,
kokote duniani, tukio la kushtukiza, linalosikitisha nakuhuzunisha kama hili linapotokea, wananchi wote huungana na kuwawamoja kama taifa na kulaani wahusika na kuwafariji waathirika wa tukiohilo. Nchini Marekani, Mgombea mmoja wa Urais wakati wa uchaguzi mkuuwa Mwaka 2012 aliishutumu Serikali kutokana na tukio la kulipuliwa kwaUbalozi wa Marekani nchini Libya. Ni wazi kuwa mgombea huyu alichukuatatizo lile kama ajenda ya kisiasa. Hata hivyo, alishutumiwa vikali na Wamarekani wenzake kwa kuelezwa kuwa ni mtu mwenye kukosa kabisamisingi ya uaminifu na uzalendo kwa taifa lake (Fundamental dishonest).Serikali inasikitishwa sana wanasiasa wa aina hii ambao wanajitokezanchini na kutafuta umaarufu wa kisiasa kwa gharama za maisha yaWatanzania. Wanasiasa na viongozi wote wajiepushe na kaulizinazochochea ubaguzi wa kidini, mifarakano ya kijamii na chuki miongonimwa Watanzania. Serikali isilaumiwe kwa hatua kali za kisheriaitakazochukua dhidi ya viongozi wa aina hii ambao maslahi yao ni muhimukuliko maisha ya Watanzania, maslahi yao ni muhimu kuliko utulivu waWatanzania na maslahi yao ni muhimu kuliko umoja wa Watanzania.
Mheshimiwa Spika,
kwa niaba ya Serikali naungana na Watanzaniawenzangu kulaani wahusika wote wa tukio hilo walioshiriki kwa njia yoyote. Aidha, Serikali kwa nguvu zake zote itahakikisha kuwa watuhumiwa wotewaliohusika na kushiriki kwa namna yoyote katika tukio hili wanasakwapopote walipo na kufikishwa katika vyombo vya sheria. Tunawatakaviongozi wa kisiasa, kidini na wananchi wote kwa ujumla kila mmoja kwanafasi yake kuwajibika ili kuhakikisha kuwa nchi yetu inaendelea kuwakisiwa cha amani na utulivu.
Mheshimiwa Spika,
mwisho nawasihi Watanzania wawe watulivu wakativyombo vya dola vikiwasaka waliohusika na shambulio hilo, kila mwenyetaarifa za kuwezesha kukamatwa wahalifu hao atoe taarifa hizo kwa Jeshila Polisi. Aidha, ninawaomba Watanzania tuendelee kukataa vitendo vyauvunjifu wa amani katika nchi yetu.
Mheshimiwa Spika,
naomba kuwasilisha.
|