.

.
.

.

.
.

.

.
.

.

.
.

.

.
.

.

.
.

.

.
.

Friday, October 7, 2011

Afrika-Asia zaungana kusomesha wanawake


  Spika wa Bunge la Tanzania Mhe. Anne Makinda akihutubia Mkutano wa Afrika-Asia 2011 leo ambapo amesisitiza elimu yenye maadili ndiyo njia pekee ya kumkomboa mwanamke  pamoja na jamii kwa ujumla. Mkutano huo  umeandaliwa na Chuo Kikuu cha Wanawake cha Sookmyung  nchini Korea Kusini ambacho kimetiza miaka mia moja na tano tangu kianzishwe 1906.

 
Wahadhiri wa vyuo vikuu, wawakilishi kutoka nchi kumi na mbili za Asia na Afrika (Korea, Tanzania, Bukina Faso, China, Vietinam, Uganda, Nigeria, Senegal, Kyrgstan, Cambodia, Pakistan na Philippine) pamoja na wanafunzi wa Sookmyung wakimsikiliza Spika Makinda.

       Spika Makinda akifuatilia kwa makini hotuba ya ufunguzi wa Mkutano iliyotolewa na Rais wa Chuo Kikuu cha Sookmyung, Dkt. Young Sil Han


      Wanafunzi wa Tanzania wanaosoma Korea katika Vyuo Vikuu mbalimbali walifika kumsiliza spika wao
 
     Baadaye Spika Makinda alipata wasaa wa kukutana na vyombo vya habari na kufafanua umuhimu wa kuwa na vyuo vikuu vya wanawake.  Hapa anaongena Avivang Tv ya Korea

Salma Dinya ni mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha St. John Dodoma ambaye alialikwa kwenye mkutano huo kuiwakilisha Tanzania kama kiongozi  kijana. Hapa anatoa mada  kwa wanafunzi kutoka vyuo vikuu vya Asia na Afrika kuhusu Tanzania.
 
Rais wa Chuo kikuu cha Sookmyung Dkt. Young Sil Han akitoa maelezo mafupi kwa wageni wake

Bolozi wa Amani Uingereza Bi Elizabeth B. de. Jong akimkabidhi Spika Makinda zawadi ya kitabu “ Global Citizen”  

Spika akiwa na mazungumzo na watanzania waishio Korea akiwaelezea hali ya nyumbani  na kuwaasa wasome kwa bidii na kurejea nyumbani.

 Spika Makinda akutana na Salma Dinya Millenium Seoul Hilton Hotel

 
Spika wa Tanzania Mhe. Anne Makinda akiwa na mwenyeji wake Dkt Han, Rais wa Chuo Kikuu cha wanawake cha Sookmyung, Korea
 
Wanafunzi wa vyuo vikuu mbalimbali Asia na Afrika wakimsikiliza Bi. Salma Dinya


Picha ya pamoja katika Hoteli ya Lotte, Seoul

Picha ya pamoja ya waratibu wa mkutano wakati wa mijadala

Picha ya pamoja ya Spika Makinda, wanafunzi wa tanzania Korea na ujumbe wa Spika

Picha ya pamoja ya Viongozi wa ngazi ya juu kutoka Afrika na Asia waliohudhuria mkutano huo

Picha ya pamoja ya viongozi vijana na wageni kutoka sehemu mablimbali

Salma na wenzake baada ya mkutano wa siku ya kwanza

Salma akitoa mada akiwa na vazi la kimasai. kila mtu alimfurahia
 
Salma akisubiri kuanza kula chakula cha jioni walichandaliwa katika hoteli ya Lotte, Seoul