Tukio la kihistoria: Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli (JPJM) akisalimiana na Waziri Mkuu Mstaafu wa Awamu ya Nne na Mgombea Urais kwa tiketi ya muungano wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) kutipa CHADEMA Mhe. Edward Ngayai Lowassa. Hii ni mara yao ya kwanza wanakutana na kusalimiana tangu Mhe. Lowassa alipotoka CCM na kuhamia CHADEMA mapema mwezi Juni mwaka 2015. Vingozi hawa walikutanishwa na tukio la sherehe ya miaka 50 ya jubilee ya ndoa ya Rais mstaafu wa awamu ya Tatu Mhe. Benjamin William Mkapa tarehe 27/8/2016 Jijini Dar es Salaam. Tukio hili lilitoke wakati nchi ikiwa kwenye sintofahamu ya kiusalama kufuti mvutano mkubwa kati ya CHADEMA, Polisi na katozo la Rais la mikutano ya vya vya siasa. CHADEMA tayari imetangaza maandamano nchi nzima kwa jina la Umoja wa Kupinga Udikteta Tanzania (UKUTA) tarehe 1/9/2016 na Polisi tayari imeyapiga marufuku maandamano hayo. |