.

.
.

.

.
.

.

.
.

.

.
.

.

.
.

.

.
.

.

.
.

Saturday, March 10, 2012

Ofisi ya Bunge yapokea rasmi nyumba mpya ya Spika kutoka Pacha Building Construction Compamny

   Mkurugenzi wa Shughuli za Bunge Bw. John Joel (kushoto)
akijadili jambo na Mkurugenzi Msaidizi wa Mipango na
Teknologia ya Mawasiliano Bw. Didas Wambura mara tu kabla
 ya makabidhiano rasmi ya nymba atakayokuwa anatumia
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania iliyoko
 eneo la Uzunguni nje kidogo ya mji wa Dodoma leo.


Muonekano wa nyumba hiyo kwa mbele. Jengo hili ambalo
litakuwa makazi ya Spika yeyote atakayeliongoza Bunge
la Tanzania lilianza kujengwa Disemba 2009 na limegharimu
 takriban sh. 1.5 bilioni. Hapakuwahi kuwa na nyumba rasmi ya
Spika wa Bunge Dodoma



Mshauri Mwelekezi (consultant) wa Pacha Building Construction
Company ( ambayo ndiyo imejenga jengo hilo) Bw. Shaban
Mwatawala (kulia) akitoa maelezo ya ujumla kabla ya
kuwapitisha viongozi wa Ofisi ya Bunge katika jengo hili.
Kulia kwake ni Mhandisi wa Miradi wa Pacha
Bw. Johanes Maganga, Mkurugenzi wa Mipango na
Teknolojia ya Mawasiliano wa Bunge Bw. Siegfied Kuwite,
 na Mkurugenzi wa Sgighuli za Bunge Bw. John Joel.

 

Bw. Siegfried Kuwite akitia saini makabidhiano hayo kwa
niaba ya Katibu wa Bunge ambaye ndiye Mshitiri (client)
wa jengo.


Bw.Shaban  Mwatawala akitia saini makabidhiano hayo
kwa niaba ya Pacha Building Construction Company.


Bwana Mwatawala akimkabidhi  Msanifu Majengo
M. F. M Msangi (kulia) anyewakilisha Wakala wa Majengo ya
 Serikali. Wakala wa Majengo Tanzania ndiye Meneja wa
Mradi huu.



Mlango wa mbele wa jengo.


Ngazi ndani ya jengo ambalo lina vyumba vinne
vya kulala, sehemu ya mapumziko, sehemu ya chakula,
maktaba na jiko.





Mazingira yanayolizunguka jengo.
 

Wadau katika zoezi zima la makabidhiano



















End