.

.
.

.

.
.

.

.
.

.

.
.

.

.
.

.

.
.

.

.
.

Monday, November 10, 2014

Rais wa Bunge la SADC na Spika wa Bunge la Tanzania Mhe. Anne Makinda aongoza Bunge la SADC kushiriki mazishi ya Rais Sata

Akiwasili kwenye viwanja vya Bunge la Zambia

Akisalimiana na rais Mstaafu wa Zambia Rupia Bunda



Rais wa Bunge la SADC na Spika wa Bunge la Tanzania Mhe Anne Makinda kwa unyenyekevu mkubwa akisalimiama na Rais mstaafu wa Zambia Mzee Kenneth Kaunda wakati wa Ibada ya Misa takatifu ya wafu kwa ajili ya marehemu Michael Sata katika Viwanja vya Bunge la Zambia





Rais wa Bunge la SADC na Spika wa Bunge la Tanzania Mhe. Anne Makinda (kulia) ni miongoni mwa viongozi mashuhuri waliohudhuria Ibada ya Misa Takatifu kwa ajili ya kumwombea aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Zambia hayati Michael Sata aliyafariki dunia tarehe 29 Oktoba 2014 nchini Uingereza. Ibada hiyo imefanyika katika viwanja vya Bunge la Zambia jijini Lusaka tarehe 10/11/2014




Msafara uliosindikiza mwili wa hayati Michael Sata katka viwanja vya Bunge la Zambia tayari kwa Ibada Misa Takatifu ya mazishi.











Makinda kumzika Sata

Makinda kuongoza ujumbe wa Bunge la SADC kumzika Rais Sata kesho Mjini Lusaka , Zambia  

Na Owen Mwandumbya, Lusaka Zambia

Rais wa Bunge la SADC ambaye pia ndiye Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Anne Makinda kesho tarehe 10 Novemba, 2014 ataongoza ujumbe wa Bunge la SADC kushiriki Misa Maalum ya kuombea mwili wa aliyekuwa Rais wa Zambia marehemu Michael Chilufya Sata katika misa maalum itakayofanyika katika viwanja vya Makumbusho Mjini Lusaka, Zambia.

Katika ujumbe huo wa Bunge la SADC, Makinda ataongozana na viongozi wengine wa Bunge hilo ambao ni Spika wa Zimbabwe Mhe. Jaji Jacob Mudenda, Spika wa Bunge la Afrika Kusini Mhe. Baleka Mbete, Spika wa Bunge la Malawi Mhe. Richard Msowoya Spika wa Bunge la Angola Mhe. Fernando da Piedade Dias dos Santos na Mwenyeji wao Spika wa Zambia Dkt. Patrick Matibini.

Kutoka secretariat ya makao makuu wa Bunge hilo, katibu Mkuu wa Bunge Bunge la SADC Dkt. Essau Chiviya ataambatana na ujumbe huo kuwakilisha sekretariati ya Bunge hilo katika Misa hiyo Maalum Mjini Lusaka, Zambia.

Kwa mujibu wa ratiba ya awali iliyotolewa na Serikali ya Zambia, Misa hiyo Maalum ya kuombea mwili wa Rais Rata itanyika kesho tarehe 10 Novemba, 2014 na inatarajiwa kuhudhuriwa na Marais kutoka kila kona ya dunia pamoja na viongozi mbalimbali wa Kimataifa watakaoziwakilisha nchi zao kabla ya kufanyika kwa mazishi yake ambayo yamepangwa kufanyika siku ya jumanne tarehe 11 Novemba, 2014 jijini Lusaka.

Sata aliyekuwa na umri wa miaka 77 alifariki tarehe 29 Oktoba, 2014  jijini London Uingereza alikokuwa akipatiwa matibabu ambapo kifo chake kilitokea siku chache baada ya Zambia kusherehekea miaka 50 ya uhuru wa nchi hiyo, sherehe ambazo hakuweza kushiriki kutokana na maradhi yaliyokuwa yakimsumbua.

 Mwanasiasa huyo mkongwe aliingia madarakani mwezi Septemba 2011 baada ya kuongoza chama chake cha Patriotic Front, na kumshinda Rupiah Banda, ambaye alikuwa rais wakati huo na chama chake cha Movement for Multi-Party Democracy, kikiwa madarakani kwa miaka ishirini.

Sata ambaye alibatizwa jina la "King Cobra" na wafuasi wake wakati alipochaguliwa mwaka 2011, alionekana kama mbadala wa siasa za Zambia na mtu ambaye alikuwa wavitendo licha ya kukosolewa kwa sehemu kubwa na upinzani.

Makinda na ujumbe wake wanatarajia kurudi nchini siku ya jumatano baada kushiriki pia mazishi yatakayofanyika tarehe 11 Novemba, 2014.

Afya ya Rais yaimarika

Dkt wa Rais Prof Mohamed Janabi (Kulia) akimfahamisha jambo Daktari Bingwa wa upasuaji Edward Shaeffer wa Hospitali ya John Hopkins iliyoko Baltimore Maryland Marekani mara kabla ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete kufanyiwa upasuaji.

Daktari bingwa Edward Shaeffer akiwa na Rais Kikwete kabla hawajaingia chumba maalum cha upasuaji

Afya ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeendelea kuimarika vizuri baada ya kufanyiwa upasuaji wa tensi dume katika Hospitali ya John Hopkins iliyoko Maryland Marekani tarehe 9/11/2014.  Tayari Mhe. Rais amenza kufanya mazoezi kuashiria hivi karibuni atarejea nyumbani na kuendelea kuchapa kazi. Tuendelee kumuombea kwa Mungu. Aliyesimama ni Mwakilishi wa Tanzania nchini Marekani Balozi Liberata Mulamula aliyefika hospitalini kumjulia hali. (Picha kwa hisani ya Michuzi Blog)


Tuesday, November 4, 2014

TAARIFA: TBC kuonyesha live Rais Kikwete anapoongea na Wazee wa Dodoma wakati wowote kuanzia sasa.



Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Profesa Jakaya Mrisho Kikwete mchana huu ataanza kuzungumza na Wazee wa Dodoma  katika ukumbi wa Kilimani mjini Dodoma wakati wowote kuanzaia sasa. Usikose kuangalia mazungumzo hayo yatayooneshwa moja kwa moja na TBC One pamoja na mtandao wa www.ikulu.go.tz

IMETOLEWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO YA RAIS IKULU,

NOVEMBA 4, 2014

Wakazi wa Dodoma wakisubiri kwa hamu kumsikiliza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya leo kupitia Supersport ndani ya DSTV.


Makinda akutana na Sekretariat ya Wakuu wa nchi za SADC, Stergomena Tax mjini Gaborone, Botswana.

Rais wa Bunge la SADC ambaye pia ni Spika wa Bunge la Tanzania Mhe. Anne Makinda akiwa katika Mazungumzo na Katibu Mkuu wa Sekretariat ya Wakuu wa Nchi za SADC Dkt. Stergomena Tax alipokutana nae kwa ajili ya mazungumzo ya kubadilishana taarifa za Bunge la SADC na Sekretariat hiyo Mjini Gaborone, Botswana jana. kushoto kwa spika ni Katibu Mkuu wa Bunge la SADC Dkt Esau Chiviya na kulia ni Katibu wa Spika Daniel Eliufoo. Dkt. Tax  aliambatana na Dkt. Angello Mondlane (kulia kwake) Mkurugenzi wa Sera na Mipango  na Mwanasheria wa Sekretariat hiyo Dr. Teodosio Uate.

Rais wa Bunge la SADC ambaye pia ni Spika wa Bunge la Tanzania Mhe. Anne Makinda akiwa katika Mazungumzo na Katibu Mkuu wa Sekretariat ya Wakuu wa Nchi za SADC Dkt. Stergomena Tax alipokutana nae kwa ajili ya mazungumzo ya kubadilishana taarifa za Bunge la SADC na Sekretariat hiyo Mjini Gaborone, Botswana jana. kushoto kwa spika ni Katibu Mkuu wa Bunge la SADC Dkt Esau Chiviya aliye kulia kwa  Dkt. Tax  ni Dkt. Angello Mondlane Mkurugenzi wa Sera na Mipango wa Sekretariat hiyo.

Rais wa Bunge la SADC ambaye pia ni Spika wa Bunge la Tanzania Mhe. Anne Makinda akiwa katika Mazungumzo na Katibu Mkuu wa Sekretariat ya Wakuu wa Nchi za SADC Dkt. Stergomena Tax alipokutana nae kwa ajili ya mazungumzo ya kubadilishana taarifa za Bunge la SADC na Sekretariat hiyo Mjini Gaborone, Botswana jana. kushoto kwa spika ni Katibu Mkuu wa Bunge la SADC Dkt Esau Chiviya aliye kulia kwa  Dkt. Tax  ni Dkt. Angello Mondlane Mkurugenzi wa Sera na Mipango wa Sekretariat hiyo.

Rais wa Bunge la SADC ambaye pia ni Spika wa Bunge la Tanzania Mhe. Anne Makinda akipokea zawadi kutoka kwa  Katibu Mkuu wa Sekretariat ya Wakuu wa Nchi za SADC Dkt. Stergomena Tax akimpongeza kuchaguliwa kwake kuwa Rais wa Bunge hilo. Mhe. Makinda alikutana na Dkt. Stergomena Tax Mjini Gaborone, Botswana jana kwa ajili ya mazungumzo ya kubadilishana taarifa za Bunge la SADC na Sekretariat hiyo jana.


Rais wa Bunge la SADC ambaye pia ni Spika wa Bunge la Tanzania Mhe. Anne Makinda akipokea zawadi kutoka kwa  Katibu Mkuu wa Sekretariat ya Wakuu wa Nchi za SADC Dkt. Stergomena Tax akimpongeza kuchaguliwa kwake kuwa Rais wa Bunge hilo. Mhe. Makinda alikutana na Dkt. Stergomena Tax Mjini Gaborone, Botswana jana kwa ajili ya mazungumzo ya kubadilishana taarifa za Bunge la SADC na Sekretariat hiyo jana.


Rais wa Bunge la SADC ambaye pia ni Spika wa Bunge la Tanzania Mhe. Anne Makinda na ujumbe wake akiwa katika picha ya pamoja na Katibu Mkuu wa Sekretariat ya Wakuu wa Nchi za SADC Dkt. Stergomena Tax pamoja na ujumbe wake Mjini Gaborone, Botswana jana baada ya mazungumzo. 
(Picha zote na Owen Mwandumbya wa Bunge)

Harakati za kisiasa kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu zapamba moto.

Ben Komba/Pwani.

Harakati za kisiasa kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu zimepamba moto kwa baadhi ya wanasiasa kujitokeza kutoka vyama mbalimbali kwa lengo la kugombea nafasi za uongozi.

Mmoja wa wanasiasa ambao nimekutana nae ambaye amenieleza kiu yake ya kugombea kiti cha Ubunge kwa tiketi ya CCM, Ni Mwalimu mstaafu BW.ISRAEL SAZIA ambaye ni Pia ni Mwenyekiti wa Kituo cha wasaidizi wa Kisheria mjini Kibaha.

BW.SAZIA amesema amechukua uamuzi huo kutokana na uzoefu mkubwa aliokuwa nao katika masuala ya siasa na amepania kuwaletea maendeleo ya kweli wana Kibaha akibahatika kuchaguliwa katika uchaguzi mkuu ujao.

Aidha amewataka wapiga kura kujiepusha na watu wanaokuja Kibaha nyakati za uchaguzi kwa lengo la kutaka kupata nafasi za kisiasa, ilihali wakiwa sio wakazi na wenyeji wa Kibaha na hivyo kushindwa kuelewa kiini cha matatizo ya Kibaha.

Wakati mgombea aliyejitokeza kugombea ubunge kwa tiketi ya CCM anajinadi, Nao UKAWA hawapo nyuma katika kuhakikisha wanatoa upinzania mkali kwa CCM ambapo Mwenyekiti wa Baraza la vijana wa CHADEMA,BW.FADHILI NGONYANI ameelezzea nia yake ya kugombea nafasi ya Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa ya Machinjioni.

BW.NGONYANI amesema wakati umefika wa kufanya mabadiliko ya ukweli ya kimfumo nchini ili kuwezesha kuharakisha harakati za kimaendeleo kwa jamii ya watanzania ambao kwa sasa wanaishi katika umaskini mkubwa.

Msaada tutani.

Ben Komba/Pwani.

Mtoto wa kike BI.ELIZABETH SAMUEL mwenye umri wa miaka 13 mkazi wa Mailimoja shule amepotea katika mazingira ya kutatanisha takriban wiki moja,mjini Kibaha mkoa wa Pwani.

Mjomba wa mtoto ELIZABETH, BW.BONIFACE KITILA amesema siku aliyopotea alikuwa amevaa sketi ya bluu ya shule na fulana ya rangi ya ugoro iliyokuwa na maandishi ya LOVE  maeneo ya tumboni akiwa bila viatu.

Bw.KITILA ameongeza kuwa mtoto huyo ambaye ni mgeni mjini Kibaha, ametokea Singida kwa lengo la kuja kuishi na shangazi yake mjini Kibaha na mpaka sasa juhudi mbalimbali zimeshafanyika ikiwa pamoja na kuripoti kituo cha Polisi.

Ametoa wito kwa wananchi kutoa taarifa kituo chochote cha Polisi watakapomuona mtoto anayefanana na na wasifa uliotolewa,au apigiwe simu namba 0765871647.

Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amemtumia Salamu za Rambirambi Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) Taifa, Bwana Sixtus Mapunda kuomboleza kifo cha Katibu wa UVCCM.




THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS

Telephone: 255-22-2114512, 2116898
Website : www.ikulu.go.tz              

Fax: 255-22-2113425



PRESIDENT’S OFFICE,
      STATE HOUSE,
              1 BARACK OBAMA ROAD,  
11400 DAR ES SALAAM.
Tanzania.
 

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amemtumia Salamu za Rambirambi Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) Taifa, Bwana Sixtus Mapunda kuomboleza kifo cha Katibu wa UVCCM Wilaya ya Arumeru, Lucy Bongele kilichotokea tarehe 2 Novemba, 2014 kwa ajali ya gari.

Ajali hiyo ilitokea katika Wilaya ya Ngorongoro baada ya gari walilokuwa wakisafiria aina ya Land Cruiser Prado Namba T380 ADP kuacha njia na kupinduka wakati Katibu huyo na Viongozi wenzake wa UVCCM walipokuwa wakienda kumsimika Bruno Kawasange kuwa Kamanda wa UVCCM Wilaya ya Ngorongoro.  Ajali hiyo iliwajeruhi viongozi wengine watano wa UVCCM pamoja na Dereva.

“Nimepokea kwa mshtuko na masikitiko makubwa taarifa ya kifo cha ghafla cha Katibu wa UVCCM Wilaya ya Arumeru, Lucy Bongele kilichosababishwa na ajali ya gari, wakati Katibu huyo alipokuwa akienda kumsimika Bruno Kawasange kuwa Kamanda wa UVCCM wa Wilaya ya Ngorongoro”, amesema Rais Kikwete katika Salamu zake.

“Kutokana na kifo cha hicho, ninakutumia Salamu za Rambirambi kutoka dhati ya moyo wangu kwa kumpoteza mmoja wa vijana hodari na wachapakazi katika safu ya uongozi ya UVCCM. Kuondoka kwake kumeacha pengo kubwa katika safu ya uongozi wa UVCCM  katika Wilaya ya Arumeru”, amesema Rais Kikwete.

“Naomba Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema aipokee na kuilaza mahala pema peponi Roho ya Marehemu Lucy Bongele. Namwomba Mola awawezesha kupona haraka majeruhi wote wa ajali hiyo  wapone haraka ili waendelee kusaidia UVCCM katika uongozi wake”, ameongeza kusema Rais Kikwete katika salamu zake.

Rais Kikwete amewaomba ndugu na jamaa wa Marehemu Lucy Bongele wawe wavumilivu na wenye subira wakati huu wanapoomboleza kifo cha mpendwa wao, na amewahakikishia kuwa yuko pamoja nao katika kipindi chote cha maombolezo.


Imetolewa na;
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu – Dar es Salaam.
4 Novemba,2014