.

.
.

.

.
.

.

.
.

.

.
.

.

.
.

.

.
.

.

.
.

Monday, May 7, 2012

Spika Makinda ahudhuria mkutano - EALA na habari nyingine


Spika wa Bunge la Tanzania Mhe. Mhe. Anne Makinda akiwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kigali Rwanda na kulakiwa na mwenyeji wake, Spika wa Bunge la Rwanda Mhe. Rose Mukantabana - ambapo atahudhuria mkutano wa saba wa maspika wa mabunge ya nchi wanachama wa Afrika Mashariki

Spika Makinda akiwa na mazungumzo na mwenyeji wake Spika Mukantabana mjini Kigali
Meneja wa Kinywaji cha Grand Malta akiwangoza wenzake kupanda miti katika kitivo cha Elimu ndani ya Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM)

Rais mstaafu Benjamin Mkapa akitoka mahakamani Kisutu jana ambapo alifika kumtetea aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Itali Balozi Costa Mahalu pamoja na Grace martini wanaoshtakiwa kwa kununua jengo la Ubalozi kinyume na taratibu

Ndoto ya Mama Tunu Pinda ya kuichangishia Timu ya Mpira wa Kikapu yavuka lengo la kiwango cha sh milioni sabini. Asanteni watanzania

Mbunge mteule wa Bunge la Afrika Mashariki Bi Shy Rose Bhanji (kulia) afika na kujitambulisha kwa balozi wa Kenya nchini Balozi Mutinda Mutiso

Friday, May 4, 2012

Keki, darasa, kazi!

Shosti karibu keki........aka kwa rangi hizo hunipati ng'o! Ilikuwa ni sherehe ya siku ya kuzaliwa Mbunge wa Afrika Mashariki Mhe. Shyrose Bahnji pamoja na marafiki zake jana.


Lilian Liundi kutoka TGNP akiwanoa wanahabari jijini dar leo


Kazi ni kazi baba  ... hakuna kuchagua kazi

Thursday, May 3, 2012

Martha Moghu ameremeta

Bi Martha Moghu (Kulia) ambaye ni mpambaji maarufu akiwa na mpambe wake jana alipoagwa rasmi (send off)  na ndugu jamaa na marafiki kati ukumbi wa Cavilum wa mjini Dodoma. Picha nyingine ni matukio mbalimbali yaliyoambatana na tukio hilo la kufana.




Tuesday, May 1, 2012

Mei Mosi, Kidato cha Sita


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete akilihutubia taifa kwenye kilele cha Siku wa Wafanyakazi duniani ambapo pamoja na mengine aliahidi kuboreshwa kwa maslahi pamoja na kuwajibishwa kwa waliotajwa kwenye taarifa ya CAG jijini Tanga jana.


Wafanyakazi wa Ofisi ya Bunge katika muonekano wa kikao cha Bunge: "Spika" akitoa mwongozo, "PM" akijibu maswali ya papo kwa papo na "Katibu" akiwa anafuatilia kwa makini, wakipita mbele Rais wakati wa maadhimisho ya Mei Mosi

Wafanyakazi Mei Mosi: Kauli mbiu..... Mfumuko wa Bei, Mishahara kidogo, maisha magumu

Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani Tanzania  Dkt Joyce Ndalichako akitoa takwimu za matokeo ya mitihani ya Kidado cha Sita jana. Ufaulu kwa mwaka huu 2012 umeongezeka kwa asilimia 0.34 ikilinganishwa na mwaka uliotangulia.


Sunday, April 29, 2012

AFRIKA MASHARIKI KUSHIRIKIANA KIULINZI




Viongozi wa nchi tano za Afrika Mashariki (Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi) wakiongozwa na Rais wa Tanzania Dkt Jakaya Mrisho Kikwete katika kusaini makubaliano ya ushirikiano wa mambo ya Ulinzi tarehe 28. April 2012 mjini Arusha.

















Kilio cha furaha: Mbunge wa Singida Mashariki Mhe. Tundu Lisu
akilia kwa furaha baada ya kushinda kesi ya uchaguzi

Mh. Tundu Lisu akitulizwa na mkewe



Semina maalum kwa Makatibu Muhtasi jijini Mwanza


Rose Mhando alivyoteka nyoyo za watu siku ya Pasaka tarehe 8.4.2012 katka Uwanja wa Taifa


Friday, April 27, 2012

NEC na maamuzi magumu!

Juu & Chini: Mwenyekiti wa CCM Taifa aliye pia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiendesha kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM Jijini Dar es Salaama ambapo maamuzi magumu ya kuliusuka upya baraza la mawaziri na kuwatosa waliotajwa na Bunge kuwa ni vikwazo kwa maendeleo ya Taifa hili. Kikao hicho kilifanyika jana.




Dkt Lina Mhando, Mhadhiri mwandamizi kutoka Marekani awapasha waafrika kuwa migogoro ya mara kwa mara, uroho wa madaraka, rushwa, uzembe na unyanyasaji wa kijinsia ndivyo vunavyolitafuna bara hili


Tuesday, April 24, 2012

Yaliyojiri



Acheni Mungu aitwe Mungu.... dhahama ya nguzo za umeme mkubwa zaidi ya 20 zaanguka Dar kutokana na upepo mkali. Hajafa mtu bali baadhi wamejeruhiwa




Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma akisherehekea harusi yake ya nne Aprili 2012

Warembo wajinoa kuwania Miss Redds, Arusha

Pamoja na fani ya usanii wataka kuongeza fani ya ufundi magari

A flower of joy


Sunday, April 22, 2012

Heshima za mwisho kwa hayati Brigedia Jenerali Mstaafu Adam Mwakanjuki 22 Aprili 2012


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya mrisho Kikwete

Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe. Dkt Mohammed Shein akisaini kitabu cha maombolezo

Rais wa Serikali ya Mapiduzi Zanzibar

Habari Mchanganyiko


Penye shimo panda mti na kuumwagilia

Mhe. Deo Filikunjombe akisaini karatasi la nia ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu. Kulia ni Mhe. Zitto Kabwe


Waziri Mkuu Mizengo Pinda akiteta jambo na wabunge wa vyama vya upinzani jana.






Meli ya uvuvi haramu "ya samaki wa Magufuli" ikielekea kuzama

Thursday, April 19, 2012

Bunge la Kumi, Mkutano wa Saba, Dodoma

Karibu kijana... muhimu tupingane bila kupigana... Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mizengo Kayanza Peter Pinda akizungumza na mbunge mpya wa Arumeru Mashariki Mhe. Joshua Nasari katika viwanja vya Bunge jana




Spika wa Bunge Mhe. Anne Semamba Mamkinda (Mb), (kushoto) akiwa na mazungumzo na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue mara Balozi huyo alipomtembela ofisini kwake Dodoma jana.






Kushoto: Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda akiwafunda Wabunge wapya wa Bunge la Afrika Mashariki waliochaguliwa hivi karibuni jinsi ya kuweka uzalendo mbele na mengine baadaye. Shughuli hii ilifanyika katika Ofisi ya Spika mjini Dodoma




Kwetu siasa si ugomvi....Makamu wa Kwanza wa Serilaki ya Mapinduzi Zanzibar aliye pia Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF) Mhe. Maalim Seif Hamad akisalimiana na hasimu wa wake Mbunge wa Wawi Mhe. Hamad Rashid Hamad jijini Dar es Salaam hivi karibuni