.

.
.

.

.
.

.

.
.

.

.
.

.

.
.

.

.
.

.

.
.

Monday, May 6, 2013

NANCY MOSHI MISS ARUSHA

Warembo Arusha mjini wakijiandaa kumsaka Miss Redds

Hali ikafikia tano Bora


Hatimaye akapatikana Bi Nancy Moshi, Miss Redds Arusha City


Kauli ya Serikali

 
KAULI YA SERIKALI BUNGENI KUHUSU MLIPUKO ULIOTOKEAKATIKA KANISA KATOLIKI LA MTAKATIFU JOSEPH PAROKIA YAOLASITI, ARUSHA MJINI TAREHE 5 MEI, 2013

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Dk. Emmanuel Nchimbi

Mheshimiwa Spika,
kwa mujibu wa Kanuni ya 49 (1) ya Kanuni zaKudumu za Bunge, Toleo la Aprili, 2013, naomba kuwasilisha Taarifa yaawali kuhusu tukio la mlipuko uliotokea katika Kanisa Katoliki la MtakatifuJoseph Mfanyakazi, Parokia ya Olasiti, Jijini Arusha tarehe 5 Mei, 2013 saa4:30 asubuhi.

Mheshimiwa Spika,
mnamo tarehe 5 Mei, 2013 saa 4:30 asubuhikulitokea mlipuko katika kanisa Katoliki la Mtakatifu Joseph Mfanyakazi,Parokia ya Olasiti, jijini Arusha. Mlipuko huo ulitokea muda mfupi baada yakuanza kwa ibada ya uzinduzi wa Parokia. Mgeni Rasmi katika uzinduzialikuwa ni Balozi wa Vatican nchini na Mjumbe wa Baba Mtakatifu, AskofuFransisco Mantecillo Padilla. Aidha, alikuwapo mwenyeji wake AskofuJosephati Lebulu wa Jimbo Kuu Katoliki Arusha. Katika uzinduzi huoinakadiriwa kuwa kulikuwa na zaidi ya watu 2000. Wakati Mgeni Rasmiakiwa ametoka nje ya Kanisa akijiandaa kukata utepe kama ishara yauzinduzi mtu alirusha kitu chenye ukubwa wa ngumi kuelekea eneo kulipokuwa na mkusanyiko wa watu ambapo baada ya kutua kulitokeakishindo na mlipuko mkubwa. Mlipuko huo ulisababisha taharuki miongonimwa waumini na kusababisha watu kukimbia ovyo.

Mheshimiwa Spika,
katika tukio hilo watu wawili wamefariki duniaambapo REGINA LONGINO KURUSEI, Mwarusha, umri wa miaka 45, mkaziwa Olasiti alifariki dunia siku ya tukio wakati akipatiwa matibabu katikaHospitali ya Mount Meru na majeruhi mwingine JAMES GABRIEL umri wamiaka 16 amefariki dunia usiku wa kuamkia tarehe 6 Mei, 2013. Aidha,watu 59 wamejeruhiwa na watatu kati yao ni mahututi. Majeruhi 38walikimbizwa hospitali ya Mount Meru kupatiwa matibabu. Majeruhi 16walikimbizwa hospitali ya St. Elizabeth kwa Father Babu, majeruhi mmojaalipelekwa hospitali ya Selian na majeruhi mwingine alipelekwa katikahospitali ya Dkt. Wanjara, Mianzini. Natumia fursa hii kutoa pole kwawafiwa, uongozi wa kanisa Katoliki, wakazi wa Arusha na Watanzania wotekwa tukio hili la kinyama. Aidha, nawaombea majeruhi wote wa tukio hilowapone haraka.

Mheshimiwa Spika,
 Viongozi wa dini na Serikali waliohudhuria ibada hiyohawakupata madhara yeyote kufuatia mlipuko huo. Baada ya Jeshi la PolisiMkoa wa Arusha kupokea taarifa ya tukio hilo waliimarisha ulinzi kwakuongeza idadi ya askari katika eneo hilo. Aidha, Kamati ya Ulinzi naUsalama ya Mkoa ikiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha MheshimiwaMagesa Mulongo walifika eneo la tukio na kufanya tathimini ya hali ilivyona kuelekeza hatua za kuchukuliwa.
 
Mheshimiwa Spika,
kutokana na uzito wa tukio hilo, kitaifa na kimataifa,Makamu wa Rais Mheshimiwa Dkt. Mohamed Gharib Bilal, Naibu Waziri waMambo ya Ndani ya Nchi, Mheshimiwa Pereira A. Silima, na InspektaJenerali wa Polisi, Said A. Mwema walikwenda Arusha na walitembeleaeneo la tukio, waliwatembelea majeruhi na kuelekeza hatua za ziada zakuchukuliwa.

Mheshimiwa Spika,
Uchunguzi wa awali unaonyesha kuwa mlipuko huoni bomu. Uchunguzi wa kubaini aina ya bomu lililotumika unaendeleakufanywa na Jeshi la Polisi na Wataalamu wa Jeshi la Wananchi waTanzania. Hadi sasa watuhumiwa sita wanashikiliwa na Jeshi la Polisi.Miongoni mwao ni Victor Calisti Ambrose
mwenye umri wa miaka 20,dereva wa bodaboda , mkazi wa Kwa Mrombo, Arusha ambayeanatuhumiwa kwa kurusha bomu hilo. Watuhumiwa wengine watanowaliokamatwa ni raia wanne wa kigeni na Mtanzania mmoja ambaowanashikiliwa kwa mahojiano.

Mheshimiwa Spika,
siku za karibuni kumekuwepo jitihada kubwa sana zawatu wachache wasiyoitakia mema nchi yetu kutaka kupandikiza chuki zakidini miongoni mwa watanzania na kuleta mapigano na mauaji miongonimwa watanzania, sina shaka kuwa shambulio la Arusha ni sehemu yamikakati hiyo miovu. Nataka niwahakikishie Watanzania kuwa Serikalihaitavumilia hata kidogo mbegu za chuki za kidini miongoni mwawatanzania na tutachukua hatua kali bila huruma kuzigandamiza njama hizimbaya dhidi ya taifa letu. Tutachukua hatua kali kwa mtu yeyote bila kujalihadhi na nafasi yake katika jamii. Amani yetu kwanza na taifa letu kwanza.
Mheshimiwa Spika,
Pamoja na kukamatwa kwa watuhumiwa hao, Waziriwa Mambo ya Ndani ya Nchi na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifawametoa maelekezo kwa Vyombo vya Ulinzi na Usalama ambapo tayariInspekta Jenerali wa Polisi kwa kushirikiana na Wakuu wa Vyombo vinginevya Ulinzi na Usalama wameunda Kikosi Kazi maalumu ili kuchunguza tukiohilo.

Mheshimiwa Spika,
kokote duniani, tukio la kushtukiza, linalosikitisha nakuhuzunisha kama hili linapotokea, wananchi wote huungana na kuwawamoja kama taifa na kulaani wahusika na kuwafariji waathirika wa tukiohilo. Nchini Marekani, Mgombea mmoja wa Urais wakati wa uchaguzi mkuuwa Mwaka 2012 aliishutumu Serikali kutokana na tukio la kulipuliwa kwaUbalozi wa Marekani nchini Libya. Ni wazi kuwa mgombea huyu alichukuatatizo lile kama ajenda ya kisiasa. Hata hivyo, alishutumiwa vikali na Wamarekani wenzake kwa kuelezwa kuwa ni mtu mwenye kukosa kabisamisingi ya uaminifu na uzalendo kwa taifa lake (Fundamental dishonest).Serikali inasikitishwa sana wanasiasa wa aina hii ambao wanajitokezanchini na kutafuta umaarufu wa kisiasa kwa gharama za maisha yaWatanzania. Wanasiasa na viongozi wote wajiepushe na kaulizinazochochea ubaguzi wa kidini, mifarakano ya kijamii na chuki miongonimwa Watanzania. Serikali isilaumiwe kwa hatua kali za kisheriaitakazochukua dhidi ya viongozi wa aina hii ambao maslahi yao ni muhimukuliko maisha ya Watanzania, maslahi yao ni muhimu kuliko utulivu waWatanzania na maslahi yao ni muhimu kuliko umoja wa Watanzania.

Mheshimiwa Spika,
kwa niaba ya Serikali naungana na Watanzaniawenzangu kulaani wahusika wote wa tukio hilo walioshiriki kwa njia yoyote. Aidha, Serikali kwa nguvu zake zote itahakikisha kuwa watuhumiwa wotewaliohusika na kushiriki kwa namna yoyote katika tukio hili wanasakwapopote walipo na kufikishwa katika vyombo vya sheria. Tunawatakaviongozi wa kisiasa, kidini na wananchi wote kwa ujumla kila mmoja kwanafasi yake kuwajibika ili kuhakikisha kuwa nchi yetu inaendelea kuwakisiwa cha amani na utulivu.

Mheshimiwa Spika,
mwisho nawasihi Watanzania wawe watulivu wakativyombo vya dola vikiwasaka waliohusika na shambulio hilo, kila mwenyetaarifa za kuwezesha kukamatwa wahalifu hao atoe taarifa hizo kwa Jeshila Polisi. Aidha, ninawaomba Watanzania tuendelee kukataa vitendo vyauvunjifu wa amani katika nchi yetu.

Mheshimiwa Spika,
naomba kuwasilisha.



KANISA KATOLIKI LATIKISWA JIJINI ARUSHA



Fadhaa ilifuata baada ya mlipuko wa Bomu


Ni mauaji, majeruhi ya kinyama: Tutafakari kama taifa

Saturday, May 4, 2013

RAIS KIKWETE APONGEZA TASNIA YA HABARI, AMPOKEA RAIS WA MADAGASCA

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitoa salamu za pongezi kwa Tasnia ya
Habari katika siku ya kuadhimisha siku ya habari duniani

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete akimpokea Rais wa Serikali ya Mpito ya Madagasca Mhe. Andry Raejolina katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere jana

Friday, May 3, 2013

HABARI MCHANGANYIKO

Kutoka Bungeni: Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Mizengo Kayanza Pinda akishauriana jambo na Jaji mstaafu Mhe. Augustino Ramadhani (kati) na Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Mathias Chikawe kwenye viwanja vya Bunge Dodoma 

Mfanyabiashara aliyefahamika kwa jina la Bwana Shirima aliyeanguka kutoka ghorofa ya 9 katika Hoteli ya Concord iliyoko Kariakoo  Jijini Dar es Salaam na kuanguka juu ya taxi hotelini hapo mchana huu





Hili ni darasa na huenda tukapata makandarasi, waalimu, madaktari, masheikh, wachungaji na raia wema kutoka katika kundi hili






 You guys don't cry, there is always tomorrow: bace-alone






The President who is a father and a husband: Obama

Wednesday, May 1, 2013

MAALIM SEIF AKUTANA NA BALOZI WA CANADA


Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad (kulia) akiwa na mazungumzo na Balozi wa Canada hapa Tanzania Bwana Alexandre Leveque ofisini kwake Zanzibar mwishoni mwa wiki

Tuesday, April 30, 2013

Camera Never Lies







Mashindano ya kwanza ya ulimbwende nchini mwaka 1967 (na kusitishwa hadi 1994)  Kilimanjaro Hotel













Mwenye nambari tano Bi Theresia Shayo aliibuka kidedea













 Huko Zanzibar nako ambako mashindano yalifanyika kwa mara ya kwanza na ya mwisho mwaka 1968 Bi Hediye Khamisi Mussa (katikati) aliibuka kidedea






 Mashindando yaliporejea tena mwaka 1994 Bi Aina Maeda (katikati) alikuwa mshindi







Bi Aina Maeda akiwa na waandaaji wa mashindano ya ulimbwende

(kwa hisani ya Michuzi Blog)

Monday, April 22, 2013

Boda-Boda yaleta balaa, Tapeli amvaa Lowassa kwenye harambee ya Kanisa Iringa



Boda-Boda Iringa ikielekea kwenye Harambee ya kanisa ambapo Mhe. Edward Lowassa alikuwa mgeni rasmi jana


Yaanguka mtaroni yajeruhi

Heka heka ya majeruhi.... dereva wa bodaboda Jafet Aser akikimbizwa Hospitali

Abira wake, Theresia Mapiu, ambaye ni muuguzi akifikishwa hospitali

Jeraha la Muuguzi Theresia Mapiu aliyekuwa anawahi kwenye harambee ya kanisa la Overcomers FM

Dereva wa bodaboda akisaidiwa na mwenzake



Wauguzi hospitali ya rufaa Iringa wakipokea majeruhi

Mhe. Edward Lowassa ( Kulia) aliyekuwa mgeni rasmi kwenye harambee hiyo uso kwa uso na tapeli la kutupwa


Kijana ambae amekuwa akiwaliza watumishi mbali mbali wa umma na watu binafsi kwa kutumia jina la waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu sera na uratibu wa bunge kijana Jonathan Wiliam Lukuvi( si jina lake halisi)amekamatwa katika hafla ya kanisa la Overcomers FM akitaka kumtapeli waziri mkuu wa zamani Edward Lowassa kupitia harambee hiyo.
Kijana huyo aliingia katika ukumbi wa St.DOminic leo katika harambee ambayo mgeni rasmi alikuwa ni Lowassa na kupita mbele na kutumia kipaza sauti kuzungumza kuwa anaitwa JOnathan Wiliam Lukuvi na ni mtoto wa waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu sera na uratibu wa bunge na kuwa amekuwa akimpigia simu mara kwa mara Lowassa na hata katika mkutano wake wa Jangwani jijini Dar es Salaam alipata kuzungumza na Lowassa na hivyo kuomba kutekelezewa ombi lake la msaada ambao hakuutaja.
Kutokana na utambulisho huo baadhi ya watu waliopata kutapeliwa na kijana huyo akiwemo mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa waliweza kuguna hali iliyopelekea askari polisi kufunguka na kumtia mbaroni kijana huyo ambae alikuwa akiweka mtego wa kumtapeli Lowassa na viongozi wengine katika hafla hiyo .
Hata hivyo baada ya polisi kumtia nguvuni kijana huyo baadhi ya watu waliotapeliwa waliweza kumtambua huku familia ya Lukuvi iliyokuwemo katika ukumbi huo ikimkana katu katu kuwa hana hata chembe ya familia na watu hawamtambui .
Kada wa CCM maarufu mkoani Iringa Godfrey Malenga Lukuvi alisema kuwa kijana huyo amekuwa akitumia jina la waziri Lukuvi kuliza watu na kuwa wengi wamekuwa wakilalamika kuhusu utapeli unaofanywa na kijana huyo na kuwa tayari alipata kukamatwa na polisi ila alitolewa .
Kwa upande wake katibu wa mbunge jimbo la Isimani ambae pia ni familia ya Lukuvi Bw Thom Malenga Lukuvi alisema kuwa amekuwa akipokea malalamiko mbali mbali kutoka kwa watu mbali mbali ambao wamelizwa na kijana huyo na kuwa siku zote alikuwa akiweka mtego ili kumnasa kijana huyo tapeli japo hakufanikiwa kumpata.
Thom ambae yupo nje ya mkoa wa Iringa kwa shughuli za kifamilia alisema kuwa alitamani sana kama angebahatika kumshuhudia kwa macho kijana huyo tapeli ila kwa kuwa yupo nje ya mkoa atajitahidi kurudi mapema mjini Iringa ili kumwona tapeli huyo.
Kwa upande wake mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa Teresia Mahongo alimweleza mwandishi wa mtandao huu wa www.matukiodaima.com kuwa pia kijana huyo alipata kufika ofisini kwake kwa ajili ya kumtapeli na baada ya kumshtukia alimtafuta waziri Lukuvi kwa simu na kuelezwa kuwa kijana huyo ni tapeli mkubwa .
Hata hivyo mwanahabari Gerald Malekela wa radio Nuru Fm alisema kuwa kijana huyo alipata kufika studio za radio hiyo kwa ajili ya kutapeli uongozi kwa kutumia jina hilo na kufika studi za radio hiyo huku akiwa na barua inayosifia watangazaji na kuomba kusaidiwa zaidi kama mmoja kati ya wasikilizaji .

Mtandao huu ulipata nafasi ya kumtafuta kwa njia ya simu waziri Lukuvi ambae mbali ya kumkana kuwa hamtambui bado alisema kuwa amepata kuwaliza watu mbali mbali kwa kutumia jina lake.
Lukuvi alisema kuwa tayari amepata kupokea malalamiko kutoka kwa mkurugenzi wa Manispaa ya Iringa na kumwagiza kumtakata na kutaka sheria ichukue mkondo wake.


"Mimi huyu kijana simtambui na wala si ndugu yangu ila amekuwa akitumia jina langu kutapeli watu na tayari alikamatwa na polisi kwa utapeli huo"


Mkuu wa mkoa wa Iringa Dkt Christina Ishengoma aliwaonya watu wanaoendelea kutapeli wengine kwa kutumia majina ya viongozi ama namna nyingine yeyote kuacha mara moja na kuwa akiwa kama mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa hatakubali kuona matapeli hao wakiendelea kulizwa watu kwa njia ya udanganyifu .

Hata hivyo aliwataka wananchi kujiepusha na wimbo hilo la utapeli kwa kuwaripoti polisi watu wanaowashukia kuwa ni matapeli .






 Akiwa tayari ametiwa nguvuni na Askari Kanzu
Picha zote kwa hisani ya Francis Godwin

Tuesday, April 9, 2013

Bunge la bajeti laanza Dodoma

 Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda, Naibu Spika Mhe. Job Ndugai wakiingia ukumbini tayari kwa mkutano wa bajeti na wa 11 wa Bunge leo tarehe 9, Aprili 2013
 Mwenyekiti wa Kamati ya Hesabu za Serikali Mhe. Zitto Kabwe na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe Lazaro Nyalandu wakiwasili Bungeni leo
Spika Makinda akiteta jambo na mbunge mara baada ya kipindi cha maswali na majibu
Waziri Mkuu Mizengo Pinda akibadilishana mawazo na makamu mwenyekiti wa CCm-Bara Mhe. Mwegulu Nchemba

Wednesday, April 3, 2013

JAJI MSTAAFU ERNEST MWAIPOPO AFARIKI DUNIA AJALINI


Marehemu Jaji Mstaafu Ernest Mwaipopo ambaye amefariki dunia jana kwa ajali ya gari akitokea Mbeya kuja Dar es Salaam. Marahemu alikuwa mjumbe wa Tume ya Maoni ya Katiba Mpya