.

.
.

.

.
.

.

.
.

.

.
.

.

.
.

.

.
.

.

.
.

Friday, March 28, 2014

Bila maombi hili la Katiba ni gumu….


       Mwenyekiti wa Bunge Maalum Mhe. Samwel Sitta akiongoza maombi maalum kabla ya kuanza kwa kikao cha Kamati ya Maridhiano jana usiku. Mhe. Sitta aliiunda Kamati hiyo ili kujadili na hatimaye kukubaliana kwenye baadhi ya mambo yaliyoshindwa kufikia muafaka Bungeni. Kushoto kwake ni Katibu wa Bunge Maalum Ndugu Yahaya Khamis Hamad.

  Maombi
o



Mwenyekiti akiendesha kikao cha Kamati ya Maridhiano.



 Makamu Mwenyekiti wa Bunge Maalum Mhe. Samia Suluhu Hassan pamoja na wajumbe wengine kwenye Kikao hicho

   Mhe. Freeman Aikaeli Mbowe  pamoja na wajumbe wengine kwenye kikao hicho



Dkt Asha-Rose Migiro pamoja na wajumbe wengine ndani ya kikao hicho


Prof. Costa Ricky Mahalu pamoja na wajumbe wenzake wakati wa kikao hicho.



Prof. Ibrahim Lipumba pamoja na wajumbe wengine katika kikao hicho



Kikao cha Maridhiano kinaendelea

Wednesday, March 26, 2014

Ikulu yatoa Rambimbi Kifo cha RC Tupa


THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS

Telephone: 255-22-2114512, 2116898
              press@ikulu.go.tz             

Fax: 255-22-2113425



PRESIDENT’S OFFICE,
      THE STATE HOUSE,
              P.O. BOX 9120,  
DAR ES SALAAM.
Tanzania.
 
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

SALAMU ZA RAMBIRAMBI ZA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, MHESHIMIWA DKT. JAKAYA MRISHO KIKWETE

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amemtumia Salamu za Rambirambi Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa  na Serikali za Mitaa (TAMISEMI)  Mhe. Hawa A. Ghasia kufuatia kifo cha Mkuu wa Mkoa wa Mara, Mhe. John Gabriel Tuppa, aliyefariki leo tarehe 25 Machi, 2014 katika Hospitali ya Wilaya ya Tarime.

Pokea rambirambi zangu za dhati na  masikitiko makubwa kufuatia   kifo cha Mhe. John Gabriel Tuppa. Ni huzuni kubwa na pigo kwa Serikali na hasa kwa Watendaji wenzake mkoani Mara ambao alikuwa akifanya nao kazi.    Marehemu John Gabriel Tuppa amefariki leo tarehe 25 Machi,2014 katika Hospitali ya Wilaya ya Tarime.

Rais pia amemwomba Mhe. Ghasia amfikishie salamu za pole kwa Mke  wa Marehemu,Watoto na Familia ya Marehemu kwa kuondokewa na kipenzi chao. Rais amesema, anaelewa machungu wanayoyapitia katika kipindi hiki kigumu kwani wamepoteza nguzo imara waliyokuwa wakiitegemea katika maisha yao.

“Hakika tumempoteza kiongozi mchapakazi ambaye amekuwa akijituma  na kuwatumikia Wananchi wake hadi dakika za mwisho za uhai wake.  Pengo aliloliacha Marehemu Tupa haliwezi kuzibika kamwe lakini hatuna budi kumwombea kwa Mwenyezi Mungu kuipumzisha roho ya Marehemu mahali pema peponi” Amina.

Taratibu na maandalizi ya mazishi zinafanywa kwa ushirikiano wa Familia, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mara na Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI.

Marehemu Tupa alizaliwa tarehe 01 Januari, 1950 na katika enzi za uhai wake amewahi kuongoza Wilaya za  Chunya, Mwanga, Bukoba, Muleba na Dodoma kabla ya kuteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mara Mwaka 2011. Ameacha Mke na watoto watano.

  
Mwisho!

Imetolewa na;

Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.

25 Machi,2014

Spika Makinda aapishwa, Kamati ya Uongozi yakutana

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano Mhe. Anne Semamba Makinda
akila kiapo cha Ujumbe wa Bunge Maalu.

Mwenyekiti Wa Bunge Maalum Mhe Samuel Sitta akimwapisha Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda
Mhe. Sitta akimkabidhi Mhe. Makinda vitendea kazi

Mwenyekiti wa Bunge Maalum Mhe. Samuel Sitta akiongoza kikao cha kwanza cha Kamati ya Uongozi baada ya kuundwa leo. Kamati hiyo inayoundwa na Wenyeviti wa Kamati za Bunge Maalum, Wajumbe wasiozidi watano wa kuteuliwa, Katibu na Naibu Katibu wa Bunge Maalum pamoja na mambo mengine inajukumu la kaundaa ratiba ya Bunge Maalum. Kushoto kwake ni Katibu wa Bunge Maalum Yahya Khamis Hamad na aliyekaa kulia ni Makamu Mwenyekiti wa Bunge Maalum Mhe. Samia Suluhu Hassan.




Naibu Katibu wa Bunge Maalum Dkt. Thomas Kashililah akitoa ufafanuzi kwa wajumbe wa kamati ya Bunge Maalum kuhusu uwezo wa kutumika kupigia kura vifaa vya kielekroniki vilivyofungwa katika ukumbi wa Bunge wakati kamati hiyo ilipokutana leo.





Wajumbe wa Kamati ya Uongozi ya Bunge Maalum wakimsikiliza kwa makini Mwenyekiti wakati wa kikao hicho.