.

.
.

.

.
.

.

.
.

.

.
.

.

.
.

.

.
.

.

.
.

Tuesday, April 30, 2013

Camera Never Lies







Mashindano ya kwanza ya ulimbwende nchini mwaka 1967 (na kusitishwa hadi 1994)  Kilimanjaro Hotel













Mwenye nambari tano Bi Theresia Shayo aliibuka kidedea













 Huko Zanzibar nako ambako mashindano yalifanyika kwa mara ya kwanza na ya mwisho mwaka 1968 Bi Hediye Khamisi Mussa (katikati) aliibuka kidedea






 Mashindando yaliporejea tena mwaka 1994 Bi Aina Maeda (katikati) alikuwa mshindi







Bi Aina Maeda akiwa na waandaaji wa mashindano ya ulimbwende

(kwa hisani ya Michuzi Blog)

Monday, April 22, 2013

Boda-Boda yaleta balaa, Tapeli amvaa Lowassa kwenye harambee ya Kanisa Iringa



Boda-Boda Iringa ikielekea kwenye Harambee ya kanisa ambapo Mhe. Edward Lowassa alikuwa mgeni rasmi jana


Yaanguka mtaroni yajeruhi

Heka heka ya majeruhi.... dereva wa bodaboda Jafet Aser akikimbizwa Hospitali

Abira wake, Theresia Mapiu, ambaye ni muuguzi akifikishwa hospitali

Jeraha la Muuguzi Theresia Mapiu aliyekuwa anawahi kwenye harambee ya kanisa la Overcomers FM

Dereva wa bodaboda akisaidiwa na mwenzake



Wauguzi hospitali ya rufaa Iringa wakipokea majeruhi

Mhe. Edward Lowassa ( Kulia) aliyekuwa mgeni rasmi kwenye harambee hiyo uso kwa uso na tapeli la kutupwa


Kijana ambae amekuwa akiwaliza watumishi mbali mbali wa umma na watu binafsi kwa kutumia jina la waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu sera na uratibu wa bunge kijana Jonathan Wiliam Lukuvi( si jina lake halisi)amekamatwa katika hafla ya kanisa la Overcomers FM akitaka kumtapeli waziri mkuu wa zamani Edward Lowassa kupitia harambee hiyo.
Kijana huyo aliingia katika ukumbi wa St.DOminic leo katika harambee ambayo mgeni rasmi alikuwa ni Lowassa na kupita mbele na kutumia kipaza sauti kuzungumza kuwa anaitwa JOnathan Wiliam Lukuvi na ni mtoto wa waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu sera na uratibu wa bunge na kuwa amekuwa akimpigia simu mara kwa mara Lowassa na hata katika mkutano wake wa Jangwani jijini Dar es Salaam alipata kuzungumza na Lowassa na hivyo kuomba kutekelezewa ombi lake la msaada ambao hakuutaja.
Kutokana na utambulisho huo baadhi ya watu waliopata kutapeliwa na kijana huyo akiwemo mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa waliweza kuguna hali iliyopelekea askari polisi kufunguka na kumtia mbaroni kijana huyo ambae alikuwa akiweka mtego wa kumtapeli Lowassa na viongozi wengine katika hafla hiyo .
Hata hivyo baada ya polisi kumtia nguvuni kijana huyo baadhi ya watu waliotapeliwa waliweza kumtambua huku familia ya Lukuvi iliyokuwemo katika ukumbi huo ikimkana katu katu kuwa hana hata chembe ya familia na watu hawamtambui .
Kada wa CCM maarufu mkoani Iringa Godfrey Malenga Lukuvi alisema kuwa kijana huyo amekuwa akitumia jina la waziri Lukuvi kuliza watu na kuwa wengi wamekuwa wakilalamika kuhusu utapeli unaofanywa na kijana huyo na kuwa tayari alipata kukamatwa na polisi ila alitolewa .
Kwa upande wake katibu wa mbunge jimbo la Isimani ambae pia ni familia ya Lukuvi Bw Thom Malenga Lukuvi alisema kuwa amekuwa akipokea malalamiko mbali mbali kutoka kwa watu mbali mbali ambao wamelizwa na kijana huyo na kuwa siku zote alikuwa akiweka mtego ili kumnasa kijana huyo tapeli japo hakufanikiwa kumpata.
Thom ambae yupo nje ya mkoa wa Iringa kwa shughuli za kifamilia alisema kuwa alitamani sana kama angebahatika kumshuhudia kwa macho kijana huyo tapeli ila kwa kuwa yupo nje ya mkoa atajitahidi kurudi mapema mjini Iringa ili kumwona tapeli huyo.
Kwa upande wake mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa Teresia Mahongo alimweleza mwandishi wa mtandao huu wa www.matukiodaima.com kuwa pia kijana huyo alipata kufika ofisini kwake kwa ajili ya kumtapeli na baada ya kumshtukia alimtafuta waziri Lukuvi kwa simu na kuelezwa kuwa kijana huyo ni tapeli mkubwa .
Hata hivyo mwanahabari Gerald Malekela wa radio Nuru Fm alisema kuwa kijana huyo alipata kufika studio za radio hiyo kwa ajili ya kutapeli uongozi kwa kutumia jina hilo na kufika studi za radio hiyo huku akiwa na barua inayosifia watangazaji na kuomba kusaidiwa zaidi kama mmoja kati ya wasikilizaji .

Mtandao huu ulipata nafasi ya kumtafuta kwa njia ya simu waziri Lukuvi ambae mbali ya kumkana kuwa hamtambui bado alisema kuwa amepata kuwaliza watu mbali mbali kwa kutumia jina lake.
Lukuvi alisema kuwa tayari amepata kupokea malalamiko kutoka kwa mkurugenzi wa Manispaa ya Iringa na kumwagiza kumtakata na kutaka sheria ichukue mkondo wake.


"Mimi huyu kijana simtambui na wala si ndugu yangu ila amekuwa akitumia jina langu kutapeli watu na tayari alikamatwa na polisi kwa utapeli huo"


Mkuu wa mkoa wa Iringa Dkt Christina Ishengoma aliwaonya watu wanaoendelea kutapeli wengine kwa kutumia majina ya viongozi ama namna nyingine yeyote kuacha mara moja na kuwa akiwa kama mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa hatakubali kuona matapeli hao wakiendelea kulizwa watu kwa njia ya udanganyifu .

Hata hivyo aliwataka wananchi kujiepusha na wimbo hilo la utapeli kwa kuwaripoti polisi watu wanaowashukia kuwa ni matapeli .






 Akiwa tayari ametiwa nguvuni na Askari Kanzu
Picha zote kwa hisani ya Francis Godwin

Tuesday, April 9, 2013

Bunge la bajeti laanza Dodoma

 Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda, Naibu Spika Mhe. Job Ndugai wakiingia ukumbini tayari kwa mkutano wa bajeti na wa 11 wa Bunge leo tarehe 9, Aprili 2013
 Mwenyekiti wa Kamati ya Hesabu za Serikali Mhe. Zitto Kabwe na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe Lazaro Nyalandu wakiwasili Bungeni leo
Spika Makinda akiteta jambo na mbunge mara baada ya kipindi cha maswali na majibu
Waziri Mkuu Mizengo Pinda akibadilishana mawazo na makamu mwenyekiti wa CCm-Bara Mhe. Mwegulu Nchemba

Wednesday, April 3, 2013

JAJI MSTAAFU ERNEST MWAIPOPO AFARIKI DUNIA AJALINI


Marehemu Jaji Mstaafu Ernest Mwaipopo ambaye amefariki dunia jana kwa ajali ya gari akitokea Mbeya kuja Dar es Salaam. Marahemu alikuwa mjumbe wa Tume ya Maoni ya Katiba Mpya